MOTO:WATU WASIOJULIKANA WARUSHA KILIPUZI KWENYE BWENI LA WANAFUNZI WA SHULE YA SDA KAHAMA.

MWONEKANO WA BWENI LA WANAFUNZI SHULE YA AWALI NA MSINGI SDA KAHAMA MARA BAADA YA MOTO KUZIMWA.

KAHAMA
 Bweni la wananfunzi wa kiume katika shule ya awali na Msingi iliyopo chini ya kanisa la wasabato katika mtaa wa Mbulu msheni mjini Kahama usiku huu limeteketea kwa moto.
 
Taarifa za awali kutoka eneo la Tukio zinasema kuwa moto huo umeanza kuwaka kutoka katika chumba cha kuhifadhia magodoro katika bweni hilo.

Akizibitisha kutokea kwa Tukio hilo Kamanda wa Zimamoto wilaya ya Kahama FRANK ELOPHAZY amesema moto huo umetokea leo majira ya saa mbili usiku na chanzo cha moto huo ni hujuma za watu kurusha kilipuzi ndani ya chumba hicho.

Samba na hilo FRANK ametoa rai kwa wamiliki wa shule zenye Mabweni kuweka uzio katika shule zao ili kulinda wanafunzi na mali zao badala ya kuweka nondo katika madirisha sanjari na kuweka mlango wa dharura.

Bweni hilo lilikuwa na wanafunzi 91 ambao wote wameokolewa huku mwalimu wa taalumu wa shule hiyo Aliyefahamika kwa jina moja la Robbinson akijeruhiwa mkono kwa kukatwa na kioo wakati wa tukio hilo.

MATUKIO KATIKA PICHA:


 MWONEKANO WA BWENI LA SHULE YA MSINGI SDA LILIVYOTEKETEA
 MIZIGO YA WANAFUNZI BAADA YA KUONDOLEWA KUTOKA KATIKA BWENI HILO.

 GARI LA SHULE YA MSINGI SDA LIKIHAMISHA VITU VYA WANAFUNZI MARA BAADA YA TUKIO HILO LA MOTO.

 MIZIGO YA WANAFUNZI ILIYOOKOLEWA KATIKA TUKIO HILO LA MOTO IKIWA NJE.
 VITANDA VILIVYOWAHIWA KUOKOLEWA VIKIWA NJE.
 WANAFUNZI WA SHULE HIYO WAKIPATA CHAKULA MARA BAADA YA ZOEZI LA KUZIMA MOTO KUMALIZIKA.

WANAFUNZI WAKIENDELEA KUPATA CHAKULA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata