WASIOKUWA NA VYOO VYA KISASA HALMASHAURI YA USHETU SASA KUKIONA CHAMOTO.
 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU MICHAEL MATOMORA.

KAHAMA
Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imesema itaanza ufuatiliaji wa kaya ambazo azijatekeleza agizo la kuwa na vyoo bora na salama baada ya muda uliotolewa wa miezi mitatu kumalizika.

Akizungumza na Kijukuu Blog Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, MICHAEL MATOMORA amesema kuwa wananchi wote wanapaswa kuwa na vyoo vyenye ubora ili kuzuia uwepo wa magonjwa ya mlipuko na atakayekaidi agizo la serikali hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

MATOMORA amesema kwa sasa halmashauri hiyo ipo katika kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo kwa wananchi hao na kuhimiza ni muhimu kila kaya kujenga choo bora na salama kwa faida yao binafsi.

Aprili mwaka huu, Halmashauri ya Ushetu ilitangaza miezi mitatu ya kampeni ya ujenzi wa vyoo bora ambapo kila kaya ilitakiwa kuwa na choo bora ndani ya kipindi hicho ambapo kaya itakayoshindwa kutekeleza agizo hilo itachukuliwa hatua za kisheria.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata