GENERALI DAVIS MWAMUNYANGE ATEULIWA KWENYE TUME YA KUCHUNGUZA GHASIA ZA BAADA YA UCHAGUZI ZIMBABWE

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnagangwa amteua Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange katika Tume ya Kutathmini athari za ghasia zilizotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Jenerali Mwamunyange ambaye alikuwa mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa miaka 10 toka 2007 mpaka alipostaafu 2017 ndio mtu pekee katika tume hiyo mwenye  ujuzi wa mambo ya kijeshi.

Mwanasheria kutoka Uingereza Rodney Dixon ambaye aliiwakilisha serikali ya Kenya katika kesi ya vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007 katika mahakama ya ICC, The Heague ni moja ya wajumbe wa tume hiyo.

Mjumbe mwengine kutoka nje ya Zimbabwe ni katibu mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Madola Chifu Emeka Anyaoku kutoka Nigeria.

Kutoka ndani ya Zimbabwe wajumbe ni Profesa Charity Manyeruke na Profesa Lovemore Madhuku kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe pamoja na Vimbai Nyemba ambaye ni rais wa zamani wa chama cha wanasheria wa Zimbabwe.

Ghasia katika uchaguzi uliofanyika Julai 30 zilisababisha vifo vya watu 6 na wengine wakiwa wamejeruhiwa.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata