APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUMWINGIZIA MTOTO UUME MDOMONI

Mkazi wa Kimara Stop Over, Riziki Joseph (37), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Dar es Salaam kwa shitaka la udhalilishaji wa kingono.

Akimsomea shitaka mbele ya Hakimu Anipha Mwingira, Mwendesha Mashtaka, Credo Rugaju, alidai Julai 24 mwaka huu maeneo ya Kimara Stop Over, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam, mshtakiwa alimdhalilisha mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba (jina limehifadhiwa) kwa kumwingizia uume mdomoni na kisha kumlawiti.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo, na kuomba kupewa dhamana kutokana na hali yake ya kiafya aliyonayo.

Hata hivyo, Hakimu Mwingira alisema dhamana iko wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu mmojawapo awe mfanyakazi kutoka taasisi inayotambulika na Serikali pamoja na bondi ya Sh 500,000.

Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana na kesi yake itatajwa tena Septemba 3, mwaka huu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata