WANAWAKE KAHAMA WANAOVAA HELMENT KWA UGESHA NA KUKAA UPANDE KUKIONA CHA MOTO.


Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani wilayani Kahama mkoani Shinyanga limesema changamoto kubwa katika vuaaji wa kofia ngumu Helment) kwenye usafiri wa Pikipiki ipo kwa wanawake ambapo wamekuwa hawatii sheria ya uvaaji wa kofia  hiyo.

Hayo yameelezwa na Afisa wa Kitengo hicho wilayani humo, Koplo DAUDI LUGOLA wakati akizungumza na Kahama fm, ambapo amesema tatizo hilo limekuwa likijitokeza mara kwa mara licha ya elimu kuendelea kutolewa.

Koplo DAUDI, amesema mbali na uvaaji wa kofia hizo, pia wamekuwa hawazingatii sheria ya ukaaji kwenye pikipiki ambapo wamekuwa wakikaa upande pamoja na kuegesha kofia hizo kwenye kichwa.

Koplo DAUDI amewataka waendesha pikipiki za abiria kuwakataa abiria wanaokataa kuvaa kofia ngumu pamoja na wanaokaa upande ili kujiepusha na kukamatwa kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata