WAMACHINGA WANAOZAGAA MITAANI KAHAMA,WATAKIWA KUFANYA BIASHARA SEHEMU MAALUMU NA WAJIUNGE KWENYE VIKUNDI ILI WAPEWE MIKOPO. MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELLACK AKIKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI MIA MOJA NA TANO KWA KIKUNDI CHA CDT SACCOSS.


KAHAMA
Wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga wanaofanya Shughuli zao katika maeneo yasiyo Rasmi wametakiwa kuondoka na kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa ili waweze kupata mikopo ya mitaji kupitia vikundi vya vijana na kinamama.

Wito huo umetolewa jana mjini Kahama na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Tellack wakati akiwakabidhi hundi ya Shilingi milioni miamoja na tano kikundi cha Kuweka na kukopa cha CDT SACCOSS.

Bi Tellack amesema kuwa vijana walioko mitaani hawawezi kupata pesa za mikopo ikiwa hawapo kwenye vikundi na kwamba halmashauri ya mji wa Kahama bado ina maeneo mengi kwa ajili ya vijana na kimama kufanya biashara zao hivyo warudi waweze kupata mikopo.

Katika hatua nyingine Bi Tellack amewataka Vijana wa CDT SACCOSS kutumia fedha walizopewa kwa miradi waliyokusudia  na kuacha kufanya biashara wazizozifahamu na walinde mitaji na kurudisha mikopo ili itumike kuwakopesha wengine.

Awali akielezea mikakati ya halmashauri kwa ajili ya vijana na kina mama,Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa  Kahama Anderson Msumba amesema halmashauri inampango wa kutoa mikopo kwa vikundi vingine na katika msimu wa kilimo ujao kila kijana atakayelima kuanzia heka tano atasaidiwa pembejeo za kilimo.

Kikundi cha vijana cha CDT Saccoss Kimeanzishwa tarehe 16/2/2018 kikiwa na jumla ya wanachama 49 ambao ni wauza matunda,Viatu vya mitumba na Urembo lengo likiwa ni kuweka akiba na kukopeshana.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata