VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA VYA PAMBA WATAKIWA KUWA WAKALI KWA WAKULIMA WAO ILI KULINDA UBORA WA PAMBA.

MWENYEKITI WA CHAMA KIKUU CHA WAKULIMA KAHAMA (KACU) EMMANUEL CHEREHANI ALIYESIMAMA AKIONGEA NA WANANCHI KATIKA SEMINA HIYO.

KAHAMA
Viongozi wa vyama vya msingi vya wakulima wa Pamba wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa wakali kwa wakulima wao ili kuhakikisha vituo vyao vinatoa pamba bora na safi katika msimu wa masoko 2017/2018.

Wito huo umetolewa leo mjini Kahama na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha wakulima Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani katika Semina Elekezi kwa viongozi wa vyama vya msing vya pamba iliyolenga kukuza uelewa katika usimamizi wa masoko.

Cherehani amesea kuwa viongozi watakapowakumbatia wakulima wao kwa vigezo vya undugu na kujuana watasababisha kukusanya pamba isiyofaa na yenye uchafu hali itakayoshusha thamnani ya pamba kwa wanunuzi.


Katika hatua nyingine Cherehani amewataka viongozi hao kuacha kuichezea mizani itakayotumika kupima pamba ili kupata uhalali wa kilo hali itayomsaidia mnunuzi kununua pamba ya halali na mkulima kupata fedha halali kutokana na mauzo ya kilo zake.

Kwa upande wao wakulima wa Pamba wameiomba Serikali kupitia Bodi ya Pamba kuwapa mikopo ya magunia ya kubebea pamba wakati wa kuvuna kama ilivyo kwa wakulima wa Tumbaku,Ili kuepuka kubeba Pamba katika vifaa vinavyosababisha Pamba kuwa chafu.

Msimu wa masoko ya Pamba kwa mwaka 2017/2018 ulianza Tarehe 1 mwezi wa tano mwaka huu na kwa Wilaya ya Kahama jumla ya kilo milioni 6 zinatarajiwa kuuzwa kutoka katika halmashauri za Kahama mji,Msalala na Ushetu.

MATUKIO KATIKA PICHA:
 WATAALMU WA ZAO LA PAMBA AMBAO NI WATOA SEMINA KATIKA MKUTANO HUO WAKIWAONYESHA VIONGOZI WA WAKULIMA WA PAMBA NAMNA YA KUTUMIA MZANI WA KIDIGITAL.

 MTAALAMU WA KILIMO AKIWAELEKEZA WAKULIMA WA PAMBA NAMNA YA KUEPUKA PAMBA KUWA CHAFU BAADA YA KUIVUNA.

 VIONGOZI WA WAKULIMA WA PAMBA WAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA MTAALAMU WA KILIMO HAYUPO PICHANI.

 VIONGOZI WA WAKULIMA WA TUMBAKU WAKIENELEA KUPATA SEMINA NAMNA YA KUVUNA PAMBA ILIYO BORA.

 VIONGOZI WA WAAKULIMA WA TUMBAKU WAKINYOOSHA MIKONO JUU ISHARA YA KUKUBALI AGIZO LA SERIKALI KUWA PAMBA YOTE IUZWE KWENYE VYAMA VYA MSINGI.

 MZEE MAARUFU WA KATA YA ZONGOMELA AMBAYE PIA NI MKULIMA WA PAMBA ALIYESIMAMA AKIULIZA SWALI KATIKA SEMINA HIYO.

 WADAU WA ZAO LA PAMBA WALIPATA NAFASI YA KUULIZA MASWALI NA KUPATA MAJIBU TOKA KWA MAAFISA USHIRIKA NA VIONGOZI WA KACU.

 MDAU AKIULIZA NAMNA WAKULIMA WAKE WATAKAVYOWEZA KUPATA MALIPO KWA NJIA YA BANK BAADA YA KUUZA PAMBA ZAO.

  AFISA USHIRIKA WA HALMASHAURI YA MSALALA AKIWAELEKEZA VIONGOZI WA WAKULIMA WA  PAMBA NAMNA YA KUTUMIA VITABU VYA KUUZIA PAMBA.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata