UNGA WA‘GYSPSUM’ WAONGEZEWA USHURU KWA ASILIMIA 10

Serikali imependekeza kuongeza asilimia 10 kwenye ushuru wa forodha kwenye unga wa gypsum kwa mwaka mmoja.

Hayo yamesemwa jana Juni 14 na Waziri wa Fedha Phillip Mpango bungeni mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka 2018/19.

Alisema marekebisho haya yanalenga  kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo hapa nchini na kuhamasisha wawekezaji watumie "gypsum' inayopatikana hapa nchini ili kuzalisha "gypsum" powder.

Alifafanua hatua hiyo inatarajiwa kuongeza ajira na mapato ya Serikali.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata