HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA YAWA MSHINDI WA KWANZA MASHINDANO YA UMITASHUMTA 2018 MKOA WA SHINYANGA.


WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAKIWA WAMEWASILI MJINI KAHAMA MARA BAADA YA KURUDI NA USHINDI WA KISHINDO KATIKA MASHINDANO YA HALMASHAURI.

 KAHAMA


Halmashauri ya mji wa Kahama Imekuwa ya Kwanza Kimkoa katika Mashindano ya UMITASHUMTA-2018 ikiziacha nyuma Halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga.

Katika mashindano hayo,Halmashauri ya Mji wa Kahama imekuwa ya kwanza ikifuatia na Halmashauri ya Kishapu.

Nafasi ya Tatu imeshikwa na Halmashauri ya Shinyanga Manispaa,huku nafasi ya nne ikishikwa na halmashauri ya Shinyanga Dc na nafasi ya tano ikishikwa na halmashauri ya Msalala.

Nafasi ya Mwisho imeshikwa na halmashauri ya Ushetu.

Kauli mbiu ya Umitashumta kwa mwaka 2018 ni michezo sanaa na taaluma ni msingi wa maendeleo ya wanafunzi katika maendeleo ya Taifa.


 MATUKIO KATIKA PICHA:
KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA CLEMENCE MKUSA ALIYESIMAMA MBELE AKIONGEA NA WANAFUNZI MARA BAADA YA KULETA KIKOMBE CHA USHINDI


WANAFUNZI WALIOSHIRIKI MASHINDANO YA UMITASHUMTA 2018 WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAKATI AKIONGEA NAO MARA BAADA YA KUMKABIDHI KIKOMBE.

MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA KUTOKA SHULE YA MSINGI NYAHANGA B DANFORD COSMAS AMBAYE NI MSHIRIKI WA MICHUANO HIYO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NAMNA WALIVYOSHINDA MICHEZO MINGI.

MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI NYAHANGA A MAUA WAZIRI AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

WALIMU NA WANAFUNZI WALIOSHIRIKI MICHEZO YA UMITASHUMTA 2018 WAKIMSILIZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ANDERSON MSUMBA MWENYE MIWANI MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA OFISI ZA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA NA KUKABIDHI KIKOMBE.

MWALIMU EDWARD YUYA KUTOKA SHULE YA MSINGI BUJIKA ALIYEONGOZANA NA WANAFUNZI HAO AKIELEEZEA MBINU WALIZOTUMIA KUPATA USHINDI HUO.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ANDERSON MSUMBA AKIONGEA NA KWA NJI YA SIMU NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MSALALA SAIMON BEREGE AKIMTANIA KWA KUSHIKA NAFASI YA PILI KUTOKA MWISHO HUKU WANAFUNZI WAKISIKILIZA NA KUCHEKA.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata