BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA TARIME VIJIJINI WAMSHUKIA MKUREGENZI WAO

Na Timothy Itembe,Tarime.
MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime vijijini mkoa wa Mara, wameelekeza  lawama kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo  Apoo Castro Tndwa kushindwa kushughulikia kero ya maji katika kituo cha Afya cha Muriba kwa muda mrefu na kusababisha wakina mama  wajawazito na watoto kukosa huduma kwa kwakati.

Madiwani hao walisema kuwa kukosekana huduma ya maji kunasababisha  kituo hicho kushindwa kufanyiwa usafi ndani ya word zao pamoja vyoo vya kusisaidia mabo kinyesi kimetapakaa nje na kuwa kero.

Akiongea kwa niaba ya wenzake huku akitolea mfano kituo hicho diwani kata ya Mriba,Michael Mgwewa alisema kuwa wajawazito na wato wanpata shida kituoni hapi pindi wanapofika ili kwenda kutafuta huduma.

'' Si mara ya kwanza kuwasilisha kero na changamoto zilizopo katika watumishi na watu wote wanaokwenda kutafuta huduma katika kituo cha Afya cha Muriba, imefikia wakati mama mjamzito na mtoto wanakosa maji ya kujiosha na hata mashuka ya kituo hicho yamebadilika rangi tofauti na rangi yake asilia nyeupe, maajabu akina mama wajawazito wanaokwenda kujifungulia katika kituo hicho cha Afya nikishuhudia wanatafuta kwa kununua katika maduka ya madawa ya binafsi Groves, hii hali ni hatari wakati Halmashauri yetu katika fedha za ndani tulivuka lengo''.alisema diwani Mugwewa.

Madiwani hao walimwagiza  mkurugenzi huyo  kutumia fedha ya dhalula kushughulikia kero hiyo ili kuondokana na tatizo linaliwakumba wakina mama na wawoto pindi wanapokuwa wameenda kutafuta huduma katika kituo hicho pamoja na vingine ndani ya halmashauri yake.

Uamuzi huo ulitolewa jana kwenye kikao cha taarifa za  kata  26 za halmashauri ya Tarime vijijini ambazo kwa pamoja ziliwasilisha kwa nyakati tofauti taarifa za utekelezaji wa mirdi ya maendeleo ambacho  kilichoongozwa na Paulo Nyangoko diwani kata ya Sirari.

na kunukuliwa na kaimu mkurugenzi wake Muraza Sebastian.
Pia pamoja na  mambo mengine madiwani hao aliendela kutupia lawama mkurugenzi  huyo kuwa alishindwa kuhakikisha vifaa tiba na dawa zinapatikana katika kituo hicho cha Afya Mriba na kwingineko hadi akina mama wajawazito wanakwenda kununua maduka binafsi ya dawa Groves baada ya kukosekana katika kituo hicho.

'' Kila leo tunaambiwa kupitia vyombo vya Habari na waziri wa Afya Ummy Mwalimu kuwa vifaa tiba na dawa vipo kila kituo cha Afya, Zahanati na Hospitali mbali mbali nchini, mbona kituo cha Afya cha Muriba hakina hata Groves hadi akina mama wajawazito wanakwenda kununua kwa pesa yao katika maduka ya madawa ya watu binafsi?'' alihoji diwani wa viti maalum kata ya Matongo Phillomena Tontora [Nyamongo].

Kwa upande wa kaimu mkurugenzi Eng wa Maji Muraza Sebastian aliwaambia madiwani hao kuwa hatua za hraka zitachukuliwa kuhakikisha huduma ya maji inapatikana iwezekanavyo ili kukiwezesha kituo hicho kitowe huduma yake ya Afya vyema watumishi wake.

Alikubliana na wazo la mpango kuanza kuvuna maji ya mvua lililotolewa na diwani wa kata ya Sirari aliyeendesha kikao hicho Pauli Nyangoko alipotoa mfano wa nchi ya jirani ya Kenya walivyopiga hatua kw njia hiyo wamepunguza kero ya maji badala ya kutegemea maji yatokanayo na uchimbaji wa visima virefu na vifupi.

Aidha Eng Muraza aliendelea kuliambia baraza hilo kuwa mganga mfawidhi wa kituo cha Afya cya Muriba hana budi kuwasilisha kero na mapungufu yaliyopo chini ya kamati yake ya Afya ziweze kushughulikiwa vilivyo katika Ofisi ya mkurugenzi zikipitia kwa mganga mkuu wa Halmashauri hiyo.

Alisema kuwa watachukua hatua za haraka iwezekanavyo kutatua kero ya upungufu wa vifaa tiba na dawa ikitangulia kufika na kukutana na uongozi wa kituo hicho cha Afya ili kubaini iweje kuchelewe utatuzi wake wakati fedha za mafungu ya uhitaji wa vifaa tiba na dawa wanazipokea mara kwa mara kupitia akaunti zao kila kituo cha Afya na zahanati.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata