WAZAZI WENYE WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA NGOZI KAHAMA WAASWA KUTOWAFICHA NDANI.

Wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) wilayani Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kutowaficha watoto wao badala yake wawape haki zao za msingi ikiwamo matibabu na elimu bila usiri wowote.

Hayo yameelezwa na  afisa tabibu wa hospitali ya Mji wa Kahama Dkt. FLORA MWINUKA wakati akiongea na KIJUKUU BLOG ambapo amesema  bado kuna baadhi ya wazazi wanawaficha watoto wao wenye ualbino licha ya elimu kuendelea kutolewa.

Amesema changamoto hiyo imekuwa ikisababisha unyanyapaa, na  kuwanyima  haki zao za msingi kama watoto wengine na kwamba jamii iache imani potovu dhidi ya watu wenye ualbino.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Wilaya ya Kahama SITA MASENYA amesema chama hicho kimekuwa kikitoa elimu kwa jamii  ili iwe tayari kuwapokea watu wenye ualbino.

Kwa mujibu wa MASENYA kwa sasa jamii wilayani Kahama imekuwa na uelewa dhidi ya watu wenye ualbino hali ambayo imepunguza matukio  ya unyanyapaa na ukatili dhidi ya watu hao katika miaka ya hivi kaaribuni.


Mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha katika maeneo mbalimbali wilayani Kahama zimekuwa zikiharibu miundo mbinu mbalimbali ya barabara na makazi ya wananchi na kusababisha baadhi yao kuzihama nyumba zao kwa muda.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata