WAZAZI HALMASHAURI YA MSALALA KAHAMA WATAJWA KUCHOCHEA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI.

 

KAHAMA
Vitendo vya wazazi na walezi kuwatuma mabinti zao kufanya biashara katika maeneo ya machimbo na kumbi za starehe vimetajwa kuchangia mimba na ndoa za utotoni katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Hayo yamebainishwa leo na baadhi ya wananchi katika kijiji cha Kalole kata ya Lunguya  halmashauri ya Msalala katika kikao cha kujadili namna ya kukomesha mimba na ndoa za utotoni kilichoandaliwa na shirika la Rafiki SDO.

Wakiongea katika kikao hicho baadhi ya wananchi hao Said Linyama,Julius Kisendi na Fatma Masaga wamesema kuwa watoto wengi hasa wakike wanatumwa na wazazi wao kufanya biashara ili kujikwamua kiuchumi katika familia zao hali inayosababisha kukumbana na vishawishi.

Naye Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Msalala Aliadina Peter amewataka wazazi na jamii kutoa malezi shirikishi kwa kuwaambia ukweli watoto wa kike kuhusu madhara ya kufanya mapenzi katika umri mdogo ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya shule.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Lunguya na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Benedicto Manuwali amelishukuru Shirika la Rafiki SDO kwa kuendelea kuwasaidia watoto wa kike kwa kuwaondoa katika machimbo na kuwapeleka katika vyuo vya ufundi.

Awali akizungumzia namna Shirika la Rafiki SDO linavyosaidia kuwalinda Watoto,Afisa wa mradi Eliud Lazaro amesema kuwa katika awamu ya kwanza waliweza kuwaondoa zaidi ya watoto 20 waliokuwa wakitumikishwa katika kazi hatarishi za Migodini.

Shirika la Rafiki SDO linatekeleza mradi wa kutokomeza Mimba na ndoa za Utotoni katika Kijiji cha Kalole halmashauri ya Msalala,Kijiji cha Mwakitolyo halmashauri ya Shinyanga vijijini pamoja na kijiji cha Iyenze Halmashauri ya Kahama mji 


MATUKIO KATIKA PICHA:
AFISA MAENDELEO YA JAMII WA HALMASHAURI YA MSALALA ALIADINA PETER AKIZUNGUMZA NA WASHIRIKI WA SEMINA YA MAFUNZO YA MALEZI NA MAKUZI NAMNA YA WAZAZI WANAVYOTAKIWA KUISHI NA WATOTO WAO.

AFISA MTENDAJI WA KATA YA LUNGUYA LUSAJO MANASE AKITOA TATHIMINI YA HALI YA KATA KATIKA MAPAMBANO YA MIMBA ZA UTOTONI.

DIWANI WA KATA YA LUNGUYA NA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MSALALA BENEDICTOR MANUALI AKITOA MIPANGO MIKAKATI YA KATA YAKE KATIKA KUTOKOMEZA MIMBA ZA UTOTONI.

WASHIRI WA MAFUNZO YA MALEZI NA MAKUZI WAKIWA MAKINI DARASANI KUMSIKILIZA AFISA MAENDELEO WA HALMASHAURI YA MSALALA.
(HAYUPO PICHANI).

MWENYEKITI WA KIJIJI CHA KALOLE HAMISI MISUNGWI AKIELEZEA JINSI WACHIMBAJI WA MACHIMBO YA MGODI YA KALOLE WANAVYOSHIRIKIANA NA SERIKALI YA KIJIJI KATIKA KUWAZUIA WATOTO KUTOFANYA KAZI NDANI YA MGODI.

AFISA KUTOKA SHIRIKA LA RAFIKI SDO ELIUD LAZARO AKIZUNGUMZA KATIKA MAJADILIANO HAYO NAMNA WANAVYOWATETEA WATOTO WANAOSHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA MARIAM MGHEN AKIWA MAKINI KUSIKILIZA MBINU ZA WAZAZI KUZUNGUMZA NA WATOTO WAO KATIKA UMRI BAREHE.

WASHIRIKI WA MAFUNZO YA MALEZI NA MAKUZI KUTOKA KIJIJI CHA TULOLE KATA YA LUNGUYA WAKIWA MAKINI DARASANI KUJADILIANA KUHUSU NAMNA YA KUMLINDA MTOTO.

BWANA SAIDI LINYAMA AKICHANGIA HOJA KATIKA MAJADILIANO YA NAMNA YA KUMUOKOA MTOTO WA KIKE KUPATA MIMBA ZA  UTOTONI.

VIONGOZI WA KATA NA KIJIJI WAKIWA KATIKA MAJADILIANO YA VIKUNDI KUHUSU NAMNA YA KUMUOKOA MTOTO WA KIKE KATIKA MIMBA ZA UTOTONI.

KAZI ZA VIKUNDI ZIKIENDELEA KATIKA SEMINA HIYO YA MALEZI NA MAKUZI

WASHIRIKI WA MAJADILIANO WAKIWA KATIKA KAZI ZA VIKUNDI HAPA WAKIJADILI MILA NA DESTURI ZINAVYOSABABISHA MIMBA ZA UTOTONI.

KAZI ZA VIKUNDI ZIKIENDELEA KATIKA SEMINA.

MMOJA WA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA MALEZI NA MAKUZI AKISOMA KIPEPERUSHI KUHUSU NAMNA YA KUMLINDA MTOTO WA KIKE.. 

MWENYEKITI WA KITONGOJI CHA CHANGALATA JULIUS KISENDI (MZEE MABANZI) AKIZUNGUMZA KATIKA SEMINA HIYO NAMNA WALIVYOJIANDAA KUWALINDA WATOTO KATIKA MACHIMBO YA NYANGALATA.

BI FATMA MASAGA MZAZI ALIYEHUDHURIA KATIKA SEMINA HIYO AKISOMA KIPEPERUSHI CHA MWONGOZO WA NAMNA YA KUMLINDA MTOTO WA KIKE.
DIWANI WA KATA YA LUNGUYA BENEDICTO MANWALI AKISIKILIZA KWA MAKINI MAJADILINO YA ELIMU YA MALEZI NA MAKUZI KWA WATOTO.

WASHIRIKI WA MAJADILIANO YA NAMNA YA KUMTUNZA MTOTO WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI AFISA MAENDELEO YA JAMII WA HALMASHAURI YA MSALALA ALIADINA PETER

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata