WAKULIMA WA TUMBAKU USHETU WALIA NA MIUNDOMBINU,WAIOMBA HALMASHAURI KUREKEBISHA BARABARA.

MENEJA MKUU WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAHAMA (KACU) MAGANGA SHIJA AKISOMA RISALA KWA NIABA YA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU USHETU.

KAHAMA
Wakulima wa zao la Tumbaku katika mkoa wa Kitumbaku Kahama wameiomba halmashauri ya Ushetu kukarabati miundo mbinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa zao hilo kutoka kwa wakulima kwenda sokoni.

Wito huo umetolewa hivi karibuni katika ufunguzi wa masoko ya Tumbaku na Meneja mkuu wa Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Maganga Shija kwa niaba ya wakulima wa zao hilo kupitia risala yao.

Shija amesema kuwa halmashauri ya Ushetu imekuwa na miundo mbinu mibovu ya Barabara hali inayokwamisha kufikisha kwa urahisi zao hilo sokoni likiwa na ubora mzuri.

Katika hatua nyingine wameomba Serikali kupitia halmashauri ya Ushetu kuboresha huduma za kijamii katika halmashauri hiyo kupitia ushuru wa tumbaku ili kuwasaidia wakulima wa tumbaku kupata huduma bora.
BARABARA KUTOKA KATA YA UBWAGWE KWENDA KAHAMA MJINI KUPITIA KATA YA ULOWA.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani ameishukuru Serikali kwa kupokea ombi la wakulima la kuanzisha bima ya mazao kwani itamsaidia mkulima kulipwa fedha zake anapopatwa na majanga kama ya mvua ya mawe.

Awali akitoa taarifa ya zao la Tumbaku nchini Mteuzi mfawidhi wa Bodi ya Tumbaku Kahama Albert Charles amesema kuwa mkoa wa kitumbaku Kahama umekuwa na mafanikio kwa miaka mitano mfulululizo kwa kuzalisha tumbaku yenye ubora kulika mikoa yote inayolima Tumbaku.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata