WAKAZI WA MTAA WA NYAHANGA KAHAMA WALIA KUJENGEWA MITARO.

Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Maliasili  mtaa wa Nyahanga halmashauri ya Mji wa Kahama wameshauri kujengwa mitaro kwenye barabara  iliyotengenezwa eneo hilo kwa kiwango cha changarawe ili kuzuia  maji ya mvua yasiharibu barabara hiyo na kwenda kwenye makazi ya watu.

Wananchi hao wametoa ushauri huo baada ya mvua kubwa iliyonyesha   wiki ilityopita kuharibu  barabara hiyo  muda mfupi baada ya  kutengenezwa kwa kiwango cha changarawe na baadae kurudiwa upya.

Wakizungumza na Kijukuu Blog wananchi hao wamepongeza hatua ya kutengeneza barabara hiyo wakisema  ili iwe imara zaidi ni lazima mitaro mikubwa  ijengwe.

Diwani wa Kata hiyo MICHAEL MAGILE amesema wamemwandikia barua Mkuu wa Wilaya ya Kahama FADHILI NKURLU kushauri hatua za  kujengwa mitaro hiyo zichukuliwe haraka ili kuinusuru barabara hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa wakala wa barabara za Mjini na vijijini (TARURA) katika halmashauri ya Mji wa Kahama Mhandisi, JOB MUTAGWABA  amesema wanakusudia kutenga bajeti kwaajili ya ujenzi wa mitaro hiyo na makaravati mengine ili kuimaraisha barabara hiyo.

Mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha katika maeneo mbalimbali wilayani Kahama zimekuwa zikiharibu miundo mbinu mbalimbali ya barabara na makazi ya wananchi na kusababisha baadhi yao kuzihama nyumba zao kwa muda.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata