WAKAZI WA MAJENGO KAHAMA WALIA NA MAFURIKO,MVUA ILIYONYESHA KWA SAA MBILI YAZUA TAHARUKI.


Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Sokola Kata ya Majengo mjini Kahama wamelazimika kuyakimbia makazi yao  baada ya  nyumba zao kujaa maji ya Mvua kubwa  iliyonyesha leo kwa muda wa saa mbili kuanzia saa tano  asubuhi hadi saa saba mchana.

Kwa Mujibu wa mwandishi wa Kijukuu Blog aliyefika eneo la tukio, Nyumba nyingi zimejaa maji ambayo yamepita katika milango hali ambayo imesababisha wananchi wakimbie makazi yao.

Wakizungumza  baadhi ya wananchi wameiomba serikali kuimarisha  mitaro ya maji ili yasiweze kuingia kwenye makazi yao  na kwamba yamesababisha uharibufu mkubwa wa samani mbalimbali za ndani ikiwamo   vyakula.

Hata hivyo wameiomba kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama kufika eneo hilo ili kujionea hali halisi na  kutoa ushauri kwa wananchi utakaokuwa msaada kwao na kwamba hakuna madhara mengine ambayo yameripotiwa hadi sasa.

Eneo hilo  limekuwa likkubwa na mafuriko  ya mara kwa mara kutokana na maji ya mvua yanayotoka sehemu mbalimbali  mjini Kahama kuelekezwa katika mtaa huo hivyo hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata