WAJASILIAMALI KAHAMA WAILALAMIKIA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA KULITELEKEZA SOKO. HILI NDILO ENEO LA SOKO LA MAJENGO AMBALO WAFANYABIASHARA WAMELIKIMBIA KUTOKANA NA UBOVU WA MIUNDO MBINU WA SOKO HILO.

KAHAMA
Baadhi ya wafanyabishara wa soko la Majengo wameilalamikia halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga kwa kushindwa kutengeneza mazingira rafiki  ndani ya soko hilo hali ambayo imesababisha meza nyingi kuwa wazi huku uchafu ukikithiri.


Wakizungumza leo na Kijukuu Blog, Wafanyabiashara hao wamedai kuwa kutokana na  ubovu wa miundombinu ndani ya soko hilo, wafanyabiashara wengi wamekimbia na kwenda kuuza bidhaa zao kwenye maeneo yasiyo rasmi.

Wakati huo  huo wamachinga wa mitumba katika soko jipya la Mitumba mjini Kahama nao wameilalamikia halmashauri hiyo kwa kushindwa kuweka mkazo wa machinga kuhamia eneo hilo licha ya kuahidiwa na serikali kuwa hakuna machinga atakayeuzia mitaani.

Baadhi ya wamachinga wamesema  nguvu kubwa imetumika kugawa viwanja katika eneo hilo ambapo kwasasa hakuna  usimamizi wowote kutoka halmashauri na kwamba ubovu wa miundombinu ya barabara katika eneo hilo ni moja  changamoto kubwa.

Kijukuu Blog imemtafuta kwa njia ya simu  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, ANDERSON MSUMBA  ambaye amesema  wameanza  kuwasaka wajasiriamali waliokaidi kuhamia kwenye masoko rasmi na  itawachukulia hatua za kisheria na kwamba usimamizi unafanyika katika masoko hayo.

MSUMBA amesema Halmashauri yake imekusudia kulifanya Soko la Majengo na  soko la Mitumba kuwa   miongoni mwa  vyanzo vya mapato baada ya kuweka miundombinu muhimu katika masoko hayo.

MATUKIO KATIKA PICHA:
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata