WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAJI KAHAMA,WASHEREHEKEA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI KWA KUPANDA MITI KWENYE BWAWA LA NYIHOGO.

 VIONGOZI WA BODI YA MAMLAKA YA MAJI KAHAMA KUWASA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA KATIKA ZOEZI LA UPANDAJI MITI KATIKA BWAWA LA NYIHOGO MJINI KAHAMA.
KAHAMA
Jamii inayozunguka bwawa la maji la Nyihogo lililopo Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuheshimu Mipaka halali iliyowekwa kwenye Bwawa hilo ikiwa ni pamoja na kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu katika eneo hilo.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa bodi wa ya maji ya mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira (KUWASA) Meja mstaafu Bahati Matala wakati wa zoezi wa upandaji wa miti katika eneo hilo katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani.

Matala amesema kuwa kwa sasa eneo hilo lina mipaka maalum hivyo wananchi hawatakiwi kuingia katika na hilo na kufanya shughuli za kibinadamu kwa kuwa bwawa hilo limetengwa kwa ajili ya matumizi ya dharula ya maji kwa wananchi wa mji wa Kahama.

Naye meneja Ufundi wa Mamlaka hiyo Mhandishi Luchanganya Paul amesema kuwa zoezi la Upandaji miti katika bwawa hilo utaisaidia kulinda mazingira ya bwawa na kulipa uhai zaidi katika siku za baadaye.

Nao baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Benard Chubwa na Grace Lukanda wamesema kuwa wamefurahi kuitumia siku ya wafanyakazi duniani kupanda miti hiyo na kutoa wito kwa wananchi kukulinda bwawa hilo kwakuwa lipo kisheria.

Viongozi wa bodi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wafanyakazi wa mamlaka hiyo Leo wamepanda miti 210 kuzungukwa bwawa la maji la Nyihogo katika kusherehekea siku ya wafanyakazi dunia.


Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yamefanyika kitaifa mkoani Iringa,Mgeni Rasmi akiwa ni  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr JOHN POMBE  MAGUFULI yakiwa na Kauli mbiu isemayo "KUUNGANISHWA KWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI KULENGE KUBORESHA MAFAO YA WAFANYAKAZI".

MATUKO KATIKA PICHA:
WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KAHAMA (KUWASA) WAKIWA ENEO LA BWAWA LA NYIHOGO WAKIPANDA MITI.

ZOEZI LA UPANDAJI MITI LIKIENDELEA KATIKA BWAWA LA NYIHOGO MJINI KAHAMA.

KILA MFANYAKAZI ALIHAKIKISHA SHIMO LAKE LINAKUWA NA MTI KATIKA KUSHEREHEKEA SIKU YA MKULIMA.

MWENYEKITI WA BODI YA MAJI MEJA MSTAAFU BAHATI MATALA AKIWA AMESHIKILIA MITI MIWILI AKITAFUTA SEHEMU YA KUPANDA KATIKA BWAWA LA NYIHOGO.

MHASIBU WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA (KUWASA) GRACE LUKANDA AKIPANDA MTI WAKE PEMBEZONI MWA BWAWA LA NYIHOGO.

ZOEZI LA UPANDAJI MITI IKIENDELEA KATIKA KUHAKIKISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI INAKUWA YENYE TIJA.

ENEO LOTE LA BWAWA LA NYIHOGO LEO LILIPAMBWA NA ZOEZI LA UPANDAJI MITI AMBAPO MITI 2010 IMEPANDWA .

WAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAJI WAKIENDELEA NA ZOEZI LA UPANDAJI WA MITI KATIKA BWAWA LA NYIHOGO.

MWENYEKITI WA BODI YA MAJI KUWASA MEJA MSTAAFU BAHATI MATALA AKIPANDA MTI KATIKA ENEO LA BWAWA LA NYIHOGO.

SURA YA TABASAMU MARA BAADA YA KUMALIZA KUPANDA MTI WAKE.

WAFANYAKAZI WA KUWASA WAKIWA BUSY NA ZOEZI LA KUPANDA MITI.

MENEJA UFUNDI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA LUCHANG'ANYA PAUL MKONOGUMO AKIWA KABEBA MITI AKITAFUTA MAHALI PA KUUPANDA PEMBENI MWA BWAWA HILO.

DEREVA WA MAMLAKA YA MAJI JOSE WHITE AKIPANDA MTI WAKE KATIKA BWAWA LA NYIHOGO MJINI KAHAMA.

MENEJA UFUNDI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA LUCHANG'ANYA PAUL MKONOGUMO AKICHIMB SHIMO KWA MAANDALIZI YA KUPANDA MTI.

ANAITWA SADOCK WILLSON MFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAJI KAHAMA (KUWASA) AKITAFUTA SEHEMU NZURI AMBAYO ANGEWEZA KUUPANDA MTI WAKE.

MZEE RAJABU LUHINDA JINA MAARUFU MZEE BUKOLI,NDIYE ANAYELINDA NA KUFANYA USAFI WA BWAWA HILO.

MARA BAADA YA ZOEZI LA KUPANDA MITI,WAFANYAKAZI NA VIONGOZI WA BODI WALIMALIZA SIKU KWA KUKAA SEHEMU MOJA NA KUPATA CHAKULA CHA MCHANA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata