TANZIA:MAMLAKA YA MAJI KAHAMA (KUWASA) YAPATA PIGO KUONDOKEWA NA MTUMISHI WAKE.

MAREHEMU REXPIRIUS VICENT 

KAHAMA
Mkazi wa Nyahanga mjini Kahama na mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Kahama mkoani shinyanga, REXPIRIUS VICENT (29) amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki iliyotokea mapema leo alfajiri katika mtaa wa Igalilimi mjini humo.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilayani Kahama DESIDERI KAIGWA amesema kuwa ajali hiyo imehusisha pipipiki aina ya boksa yenye namba za usajili T (40403), aliyokuwa akiendesha Marehemu VICENT.

KAIGWA amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva pamoja na kutokuvaa kofia ngumu na ametoa rai kwa watumiaji wa vyombo vya moto hususani pikipiki kuvaa kofia ngumu ili kuchukua tahadhari pindi ajali inapotokea.

Msemaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mji Kahama (KUWASA), JOHN MKAMA pamoja na kueleza jinsi walivyopokea taarifa ya msiba huo amesema taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika na kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea kwao mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.


Jeshi la Polisi wilayani Kahama limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa kichanga hicho kwaajili ya kwenda kuuhifadhi  kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Mji wa Kahama pamoja na  taratibu zingine.

Matukio ya kutelekeza na kutupa watoto katika wilaya ya Kahama yamekuwa yakijitokeza Mara kwa mara ambapo mapema mwezi huu, mtoto mchanga mwingine aliokotwa akiwa hai katika shamba moja kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu Halmashauri ya Msalala.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata