SERIKALI YAPONGEZA JUHUDI ZA WAKULIMA WA TUMBAKU KAHAMA,YATOA WITO WA UJENZI WA KIWANDA CHA SIGARA USHETU.


MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELLACK AKIZUNGUMZA NA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU KATIKA KATA YA UYOGO HALMASHAURI YA USHETU.

KAHAMA
Wakulima na wadau wa zao la Tumbaku katika mkoa wa kitumbaku Kahama,Wameshauriwa kujenga kiwanda cha Sigara  katika halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga ili kujihakikishia Soko la zao hilo katika siku zijazo.
 
Wito huo umetolewa leo na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ZAINAB TELLACK wakati wa ufunguzi wa masoko ya Tumbaku uliofanyika katika kata ya Uyogo halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.

Bi TELLACK amesema kuwa  wakulima wa tumbaku wakiungana wana uwezo mkubwa wa kujenga kiwanda cha Sigara hata cha ukubwa wa kati hatua ambayo amesema itasukuma mbele maendeleo yao binafsi, wilaya ya Kahama na Taifa kwa ujumla.

Sambamba na hayo TELLACK ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya Ushirika kuwa waadilifu na waaminifu katika uongozi wao na kuacha tabia ya wizi wa mali za ushirika na kuwanyanyasa wanachama waliowaweka madarakani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini,  Dkt TITUS KAMANI ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo amewataka wakulima wa Tumbaku na Pamba kudumisha ushirika kwani utawasaidia kuweka nguvu ya pamoja katika kufikia mafanikio.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) EMMANUEL CHEREHANI ameiomba Serikali kufikiria upya kuhusu utaratibu wa kununua  Tumbaku kwa fedha za kigeni kwani kununua  kwa shilingi ya Tanzania kunasababisha wakulima kupoteza Fedha nyingi.

Mkoa wa kitumbaku  Kahama umekuwa wa kwanza kufungua masoko ya zao la Tumbaku Nchini ambapo kwa msimu wa mwaka 2017/2018 jumla ya kilo Milioni 8 na Elfu 11 zitauzwa katika mkoa wa kitumbaku Kahama.

MATUKIO KATIKA PICHA:


MWENYEKITI WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAHAMA (KACU) EMMANUEL CHEREHANI AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO AMBAPO ZAIDI AMEIOMBA SERIKALI KUWAINGIZA WAKULIMA WA TUMBAKU KATIKA MFUMO WA BIMA YA AFYA.

BAADHI YA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU KATIKA KATA YA UYOGO WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MWNYEKITI WA KACU HAYUPO PICHANI.

MKULIMA WA TUMBAKU AMBAYE NI MWANAMKE KUTOKA CHAMA CHA MSINGI UYOGO AKIHAKIKISHA MAUZO YA TUMBAKU YAKE KATIKA MOJA YA GHALA LILILOPO KATIKA KATA YA UYOGO.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU MICHAEL MATOMOLA NAYE ALIKUWEPO KATIKA UFUNGUZI WA MASOKO YA TUMBAKU KATIKA HALMASHAURI YAKE.

BAADHI YA VIONGOZI NA WAKUU WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA HAYUPO PICHANI.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELLACK KULIA AKITETA JAMBO NA MWENYEKITI WA KACU MR EMMANUEL CHEREHANI.

MENEJA WA BENKI YA CRDB TAWI LA KAHAMA LUTHER MNENEY AMBAYE NI MDAU MKUBWA WA ZAO LA TUMBAKU KATIKA KUWAKOPESHA WAKULIMA NAYE ALIKUWEPO 

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ZAINABU TELLACK AKISIKILIZA KWA MAKINI HISTORIA YA ZAO LA TUMBAKU ILIYOSOMWA MBELE YAKE NA BODI YA TUMBAKU TANZANIA (TTB).

    MTEUZI MFAWIDHI WA BODI YA TUMBAKU KAHAMA  ALBERT CHARLES AKITOA HISTORIA YA ZAO LA TUMBAKU MBELE YA MKUU WA MKOA WA SHINYANAGA BI ZAINAB TELLACK. 

VIONGOZI WA VYAMA VYA MSINGI KUTOKA MAENEO MBALI MBALI NAO WALIKUWEPO KATIKA TUKIO LA UFUNGUZI WA MASOKO YA TUMBAKU.

MENEJA MKUU WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAHAMA (KACU) MAGANGA SHIJA AKISOMA RISALA YA WAKULIMA MBELE YA MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELLACK.

MWAKILISHI WA KAMPUNI YA ALLIANCE ONE DAVID MAYUNGA AKIZUNGUMZA NA WAKULIMA WA TUMBAKU KATIKA MKUTANO HUO,ZAIDI AMEKEMEA TABIA YA WAKULIMA WA TUMBAKU USHETU KUWATUMIKISHA WATOTO KATIKA UZALISHAJI WA KILIMO HICHO.

MENEJA WA MKOA WA KAMPUNI YA TLTC KAHAMA MALISELI MASARE AKIZUNGUMZA NA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU KATIKA KATA YA UYOGO ZAIDI AMEWATAKA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU KUFUNGA TUMBAKU ZAO KWENYE VITUO RASMI VILIVOSAJILIWA.

MWENYEKITI WA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA DKT TITUS KAMANI AKIONGEA NA WAKULIMA WA TUMBAKU KATIKA KATA YA UYOGO,AMEWATAKA WAKULIMA WA PAMBA NA TUMBAKU KUDUMISHA USHIRIKA AMBAO UTAWAPA NGUVU KATIKA KUJADILI MAFANIKIO YA KILIMO CHAO.

BAADHI YA VIONGOZI WA VYAMA VYA MSINGI WALIOUDHULIA KATIKA MKUTANO HUO WA UFUNGUZI WA MASOKO YA TUMBAKU USHETU WAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA HAYUPO PICHANI.

TUMBAKU YA KWANZA KUUZWA KATIKA MSIMU WA MASOKO WA MWAKA 2017/2018 IKIWA GHALANI KATIKA MOJA YA GHALA LILILOPO KATIKA KATA YA UYOGO.

MWAKILISHI WA CHAMA CHA MSINGI NGOKOLI AKIPOKEA CHETI CHA CHAMA KILICHOFANYA VIZURI KATIKA MSIMU WA KILIMO 2017/2018

MWENYEKITI WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAHAMA (KACU) EMMANUEL CHEREHANI AKIPOKEA CHETI CHA MKULIMA BORAWA TUMBAKU  KWA MSIMU WA MWAKA 2017/2018 

MWENYEKITI WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAHAMA (KACU) EMMANUEL CHEREHANI AKIPEANA MKONO NA MGENI RASMI AMBAYE NI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELLACK MARA BAADA YA KUKABIDHIWA CHETI.
 
MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELLACK AKIPOKEA MAELEKEZO YA UBORA WA TUMBAKU ILIYOINGIZWA SOKONI.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELLACK AKINDIKA DARAJA LA TUMBAKU ISHARA YA KUFUNGUA RASMI SOKO LA TUMBAKU.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BI ZAINAB TELLACK AKIENDELEA KUJAZA GRADE ZA TUMBAKU KATIKA UFUNGUZI WA SOKO.
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata