NSSF YATOA UFAFANUZI SAKATA LA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI BUZWAGI KUANDAMANA KWENYE OFISI ZAO KAHAMA.


Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa NSSF unaendelea na uhakiki  wa    madai  ya  wafanyakazi zaidi ya 200 waliokuwa kwenye  makampuni ya Pan Afrika na Pangea katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wilayani Kahama  ili kuwalipa mafao yao ya kujitoa kwenye mfuko huo.

Taarifa iliyotolewa leo na idara ya masoko na uhusiano NSSF kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa  kutokana na wingi wa madai ya wanachama hao na kiwango kikubwa  cha fedha NSSF imelazimika kuchukua hatua hiyo ya haraka.

Wiki hii baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi waliandamana hadi kwenye ofisi za NSSF mjini Kahama wakiishinikiza serikali kuingilia kati suala la kulipwa kwa haraka mafao yao ya kujioa ili kuendeleza miradi yao baada ya kutoka kwenye ajira.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata