MBUNGE WA SHINYANGA MJINI ACHAGULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP).


Taarifa hiyo imetolewa leo asubuhi Mei 11, 2018 bungeni mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge na kubainisha kuwa mbunge huyo kijana amechaguliwa jana kwa kishindo.

“Umelipa Bunge letu sifa na Tanzania kwa ujumla. Nafasi hii ni ya kuitangaza nchi yetu na Bunge hili tunamtakia kazi njema,” amesema Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi (CCM).

“Nampongeza sana kijana huyu, lakini pia Serikali kwani huwezi kupata nafasi hii kubwa kama huungwi mkono na Serikali. Nimpongeze sana Rais John Magufuli.”
Mheshimiwa Stephen Masele akiwa na Watanzania waishio Afrika KusiniSAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata