MAMA ATUPA KICHANGA CHA SIKU MOJA KANDO YA KARAVATI MTAA WA NYAKATO KAHAMA.

Mtoto mchanga   wa kiume anayekadiriwa kuwa wa siku ameokotwa akiwa amefariki dunia  kandokando ya  karavati lililopo Mtaa wa Nyakato  Kata ya Nyasubi jirani na kituo cha Mafuta cha Front oil mjini Kahama  na mwanamke ambaye hajafahamika majina wala makazi yake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Kichanga  hicho ambacho kinasadikiwa kimetupwa  tangu majira ya asubuhi leo kimeokotwa majira ya saa tisa  alasiri.

Wakizungumza na Kijukuu Blog, mashuhuda hao wamesikitishwa na kitendo hicho huku wakiomba  hatua kali zichukuliwe dhidi ya mwanamke atakayebainika kutenda unyama  huo.

Diwani wa Kata ya Nyasubi, ABEL SHIJA ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa  viongozi wa serikali  na jeshi la Polisi ambao wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo  na na kusema kwamba kitendo cha kutupa mtoto  hakina tija kwa jamii.

Jeshi la Polisi wilayani Kahama limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa kichanga hicho kwaajili ya kwenda kuuhifadhi  kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Mji wa Kahama pamoja na  taratibu zingine.

Matukio ya kutelekeza na kutupa watoto katika wilaya ya Kahama yamekuwa yakijitokeza Mara kwa mara ambapo mapema mwezi huu, mtoto mchanga mwingine aliokotwa akiwa hai katika shamba moja kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu Halmashauri ya Msalala.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata