MADIWANI MSALALA KAHAMA WAMKATAA MZABUNI ANAYESAMBAZA DAWA KWENYE ZAHANATI.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MSALALA SAIMON BEREGE

KAHAMA
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama limeazimia kuvunja mkataba  na kampuni ya BAHARI PHAMACY ndani ya siku 14 kuanzia leo baada ya kampuni hiyo kushindwa kutekeleza zabuni ya kusambaza dawa kwenye zahanati na vituo vya afya  katika halmashauri hiyo.

Akitangaza hatua hiyo katika kikao cha baraza la Madiwani, mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, SIMON BEREGE  amesema watazingatia sheria za kuvunja mkataba  na mzabuni huyo na kwamba  zabuni zijazo zitatolewa kwa muda wa majaribio ili kupima uwezo  na utendaji kazi wa mzabuni.

Akizungumza katika kikao hicho, Diwani wa kata ya Isaka, GERALD MWANZIA amesema Mzabuni huyo ameshindwa kuzingatia mkataba unavyoelekeza huku diwani wa kata ya Busangia, ALEXANDER MIHAYO akiitaka serikali kuchukua hatua stahiki.

Naye katibu tawala msaidizi, serikali za mitaa, Mkoa wa Shinyanga, ALPHONCE KASANYI amesema  atayafikisha maazimio ya baraza hilo la Madiwani la Halmashauri ya Msalala kwenye ngazi ya mkoa kwaajili ya utekelezaji.SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata