KIDATO CHA SITA KUANZA MTIHANI WAO LEO

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema watahiniwa 87,643 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita unaoanza leo Mei 7, 2018.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema leo Mei 6, 2018 kuwa mtihani utahitimishwa Mei 25, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kati yao watahiniwa hao, wa shule ni 77,222 na wa kujitegemea ni 10,421.

Dk Msonde amesema mtihani utafanyika sambamba na wa kozi ya ualimu ambao watahiniwa 7,422 wa ngazi ya cheti na stashahada wamesajiliwa kuufanya.

"Maandalizi kwa ajili ya mitihani ya kidato cha sita na ualimu yamekamilika, ikiwamo kusambaza vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mitihani hii," amesema Dk Msonde.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata