JOHN HECHE AIWAKIA SERIKALI UWEKAJI VIGINGI VIJIJINI

Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema), ameionya serikali kama haitasitisha uwekaji wa vigingi katika maeneo ya vijiji vinavyopakana na hifadhi inaweza kusababisha machafuko wilayani Tarime.

Heche ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo Mei 22, alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Kwa mujibu wa Heche uwekaji huo wa vigingi unawekwa katika vijiji vinavyotambuliwa kisheria tangu enzi za utawala wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

“Aidha, ukamataji wa mifugo inayodaiwa kuingia katika hifadhi za taifa, utaratibu huo haukubaliki kwa kuwa baadhi ya mifugo inakamatwa na kuingizwa katika hifadhi hizo na watumishi wa TANAPA na kisha kutozwa faini kubwa zisizoweza kulipika kwa haraka,” amesema Heche.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata