IDARA YA AFYA MACHIMBO YA DHAHABU KABELA ILINDI YATOA AGIZO LA KUJENGA VYOO.

Idara ya Afya na  usafi wa Mazingira katika machimbo ya dhahabu ya Kabela Ilindi, Kata ya Zongomela wilayani Kahama  imeiagiza kampuni ya  Kalyango Gold Mine kujenga vyoo vingi zaidi ili kuzuia mlipuko wa magonjwa unaoweza kujitokeza.

Akizungumza na Kijukuu Blog,  Mkuu  wa idara ya afya na usafi wa mazingira katika katika machimbo hayo, MACHIMU NELSON amesema  idara yake imajizatiti kuhakikisha kila machimbo yanakuwa na vyoo vya kutosha.

Naye Meneja wa Kampuni ya Kalyango Gold Mines,  MDAKI SHABAN amesema tayari wameanza kujenga matundu mawili ya vyoo na bafu na kwamba wanaendelea kutenga fedha zaidi kwa ajili ya kuongeza  matundu mengine  ya vyoo.


Naye Msimamizi wa  idara ya Afya na usafi wa mazingira  katika machimbo hayo ya dhahabu ya Kabela Ilindi, DANI  MUSSA amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi waishio  kwenye machimbo  ili kuimarisha usafi wa mazingira katika machimbo hayo kwa manufaa ya jamii nzima.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata