HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA YAANZA KUEZEKA MABOMA YA MADARASA YALIYOJENGWA NA WANANCHI.

Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga imeanza kuyaezeka maboma ya madarasa kwa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi ili kupunguza tatizo la uhaba wa    vyumba vya madarasa kwa shule za msingi katika halmashauri hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Elimu Shule za Msingi katika Halmashauri hiyo,  ALUKO LUKOLELA, amesema hadi sasa  vyumba vya madarasa  200  vimetengewa bajeti na kati ya hivyo  vyumba 40  vimeanza kuezekwa.

LUKOLELA, amesema Halmashauri ya Mji wa Kahama inakabiliwa na upungufu  wa vyumba vya madarasa 1300 ya shule za Msingi na kwamba baada ya kukamilika vyumba  hivyo 200 upungufu utakuwa ni zaidi ya vyumba 1100.

Mmoja wa wananchi AISHA MSANGI NAKYOO, ambaye amejitolea kujenga vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Msingi Nyahanga B, amewataka wadau kuendelea kuchangia ujenzi huo na ameitaka halmashauri kumalizia haraka madarasa yanayojengwa ili wanafunzi wayatumie.


Diwani wa Kata ya Nyahanga, MICHALE MAGILE amesema kukamilika kwa vyumba hivyo vya madarasa katika shule ya Msingi Nyahanga B, kutasaidia kupunguza tatizo la msongamano wa Wanafunzi madarasani.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata