Breaking: MBUNGE KISHOA APATA AJALI DODOMA

Mbunge wa viti maalumu (CHADEMA) wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Jesca Kishoa amepata ajali Jijini Dodoma leo Ijumaa Mei 11,2018 majira ya saa nne asubuhi. 

Akitoa taarifa za awali Afisa Habari wa CHADEMA Bw. Tumaini Makene amesema kwamba Mh. Kishoa amepata ajali asubuhi kwa kugongana na gari ndogo aina ya Pick Up alipokuwa njiani akielekekea kwenye majukumu yake ya kibunge.

Makene ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea katika njia panda ya Area D mkoani huko.

Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa Mh. Kishoa yupo katika Zahanati ya Bunge akipatiwa matibabu na uangalizi wa awali na kwamba wanasubiri kupata taarifa za Madaktari ili kujua hatua zaidi.

Kwa upande wa Mume wa Mbunge huyo, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila pia amethibitisha kutokea kwa ajali hiyoSAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata