BENKI YA AZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA MFUKO WA PSPF WATOA SEMINA KWA WASTAAFU KAHAMA.


MENEJA WA BIDHAA ZA MIKOPO KUTOKA BENK YA AZANIA MAKAO MAKUU,  THOBIAS SAMWEL AKIONGEA MBELE YA WASTAAFU KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.
KAHAMA
BENKI ya Azania kwa kushirikiana na mfuko wa hifadhi ya jamii wa  PSPF   leo (May 9) imetoa  semina  ya elimu ya pesa kwa wastaafu na wanaotarajia kustaafu hivi karibuni lengo ni kuwajengea uelewa wa kutumia pesa za mikopo  kwenye miradi ya uzalishaji mali.

Akizungumza  kwenye semina hiyo iliyohudhuriwa na mamami ya wastaafu, Meneja wa bidhaa za mikopo kutoka benk ya Azania makao makuu,  THOBIAS SAMWEL  amesema baadhi ya wastaafu wamekuwa hawatumii vizuri mikopo na mafao wanayoyapata hivyo kusababisha kuingia kwenye madeni.

SAMWELI amewashauri wastaafu kutokimbilia kuchukua mikopo kwenye taasisi za kifedha kama hawajajiandaa kufanya shughuli za uzalishaji na badala  wapate kwanza elimu ya kutosha pamoja na kubuni miradi yenye kuzalisha fedha hiyo.

Sambamba na hayo amewataka wastaafu kufungua akaunti maalum ya wastaafu katika benki ya  Azania ili waweze kupitishia pensheni zao za kila mwezi na kuwawezesha kupata mikopo kutoka benki hiyo.

Akizungumzia ubora wa akaunti hiyo,Samwel amesema hakuna kiasi cha lazima cha kufungulia akaunti,Hakuna makato ya lazima ya kila mwezi sambamba na kupatiwa Kadi ya ATM bure.

Akiongezea ubora wa akaunti hiyo Samwel amesema hakuna kiasi cha lazima cha kubaki kwenye akaunti pamoja na kuunganishwa na na huduma kupitia simu za mkononi ili kufanya miamala ya kibenki.

Naye mwakilishi wa PSPF mkoa wa Shinyanga  GWAMAKA KITOMALE amesema Mfuko huo umekuwa ukiwaelekeza wastaafu waliojiunga na mfuko huo jinsi ya kutumia  mafao yao kwa kusahihi.


Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo, wamesema kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuwa na matumizi sahihi ya  mikopo wanayoihitaji na kuishukuru benki ya Azaznia kwa kuandaa semina hiyo.

MATUKIO KATIKA PICHA:

BAADHI YA WASTAAFU NA WATUMISHI WANAOJIANDAA KUSTAAFU WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA SEMINA ILIYOKUWA INATOLEWA NA MTAALAMU WA BENKI YA AZANIA.

MEZA KUU KATIKA SEMINA HIYO IKIWA MAKINI KATIKA KUHAKIKISHA ELIMU STAHIKI INAWAFIKIA WAZEE WASTAAFU WA MJI WA KAHAMA NA VIUNGA VYAKE.

WAZEE WASTAAFU NA WATUMISHI WANAOKALIBIA KUSTAAFU WAKIFUATILI AKWA MAKINI NAMNA BENKI YA AZANIA INAVYOTOA MKOPO KWA WASTAAFU.

MEZA KUU IKIENDELEA KUTOA ELIMU KWA WASTAAFU WALIOFIKA KATIKA SEMINA HIYO ILIYOFANYIKA KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

WATUMISHI WASTAAFU WAKIWA UKUMBINI WAKISILIKIZA KWA MAKINI ELIMU KUHUSU MIKOPO KUTOKA KWA AFISA WA BENKI YA AZANIA HAYUPO PICHANI.

SEMINA IKIENDELEA KWA WASTAAFU

MWALIMU MSTAAFU MZEE ABEDI JUMA AKIULIZA SWALI KUHUSU FAIDA ATAKAZOZIPATA AKIFUNGUA AKAUNTI YA WASTAAFU KWENYE BENKI YA AZANIA.

SEMINA IKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

MMOJA WA WASTAAFU AKIULIZA SWALI KWA MAAFISA WA BENKI YA AZANIA NA MAAFISA WA PSPF,

BAADHI YA KINA MAMA WASTAAFU NA WANAOTARAJIA KUSTAAFU SIKU ZA KARIBUNI WAKIFUATILIA KWA MAKINI SEMINA HIYO ILIYOTOLEWA NA BENKI YA AZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA MFUKO WA PSPF

MENEJA WA BIDHAA ZA MIKOPO KUTOKA BENK YA AZANIA MAKAO MAKUU,  THOBIAS SAMWEL KUSHOTO AKIWA NA MWAKILISHI WA PSPF MKOA WA SHINYANGA MR GWAMAKA.

SEMINA IKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.BWANA GWAMAKA KITOMALE MWAKILISHI WA PSPF SHINYANGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA SEMINA.

MR PETER DEUS MAGANGA AFISA WA BIASHARA WA BENKI YA AZANIA KUTOKA MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA SEMINA YA WASTAAFU .

MWALIMU ANAYETARAJIA KUSTAAFU SIKU ZA USONI AKIONGEA NA KIJUKUU BLOG MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA SEMINA.

MMOJA WA WASTAAFU AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA SEMINA.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata