APANDISHWA KIZIMBANI KAHAMA KWA KUJIFANYA AFISA UHAMIAJI NA KUSAINI FOMU ZA NIDA.Mkazi wa Nyikoboko ELISHA ZEPHANIA (21) wilayani Kahama amefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma ya kujifanya mtumishi wa Serikali kinyume na sheria.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo EVODIA KYARUZI, mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi EVODIA BAIMO amesema ZEPHANIA alikamatwa May 19 mwaka huu saa 8 mchana huko Nyikoboko katika Halmashauri ya Msalala.

BAIMO amesema ZEPHANIA akiwa katika maeneo hayo alijiwasilisha kwa THOMAS PAUL na YUSTINA SIMON kua ni afisa uhamiaji na kusaini fomu za NIDA.

BAIMO ameongeza kuwa  ZEPHANIA alitenda kosa hilo la kujiwasilisha kama mtumishi wa Umma kinyume na kifungu cha sheria cha 100 na 35 kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2002.

Katika shauri hilo la jinai namba 198/2018 ZEPHANIA amekana kuteenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana hadi June 12 mwaka huu shauri hilo litakapotajwa tena mahakamani hapo.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata