WAZIRI ASEMA HAKUNA UPENDELEO UTEUZI WA MABALOZI

Tanzania ina mabalozi 40 duniani kote na kati ya hao, wanaotoka Zanzibar wako tisa, sawa na asilimia 22.5 ya mabalozi wote nchini.

Hayo yameelezwa leo Aprili 12 bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Suzan Kolimba.

Dk Kolimba amesema uteuzi wa mabalozi hufanywa kwa weledi mkubwa kwa kuangalia uwezo wa mtu.

Alikuwa akijibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (CCM), Jaku Hashim Ayoub aliyetaka  kujua Tanzania ina mabalozi wangapi wanaotoka Zanzibar huku mbunge wa Viti Maalum kutoka Zanzibar (Chadema) Mariam Msabaha akihoji kwa nini mabalozi kutoka Zanzibar wanapelekwa nchi za Uarabuni pekee.

Lakini Serikali ilikanusha madai kuwa mabalozi wanaoteuliwa kuwakilisha Tanzania wakitokea Zanzibar, wanapelekwa Uarabuni tu.

Dk Kolimba amesema hakuna upendeleo wa aina yoyote katika kuwapanga mabalozi bali kinachotazamwa ni namna ambavyo mhusika atasaidia kujenga mahusiano mema na mataifa husika.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata