WATU WASIOJULIKANA WATELEKEZA MAGODORO 30 KITUO CHA AFYA KAHAMA,DIWANI ATAKA YAPIMWE NA KUONDOLEWA KATANI KWAKE.

DIWANI WA KATA YA MWENDAKULIMA PIUS EMMANUEL AKITOA HOJA YA MAGODORO KATIKA BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA

KAHAMA
Wananchi wa kata ya mwendakulima  halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga wameingiwa na hofu baada ya magodoro 30 kutelekezwa katika  kituo  cha afya  Mwendakulima huku haijulikana  aliyeyapeleka hapo.

Akizungumza leo kwenye  kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, Diwani wa Kata ya mwendakulima Pius Emmanuel alisema  magodoro hayo yana muda mrefu sasa tangu yapelekwe katika kituo hicho cha afya  na kwamba taarifa zinadai kuwa gari ambayo haijajulikana ni ya kampuni gani ilifika eneo hilo na kuyashusha magodoro hayo na kuondoka pasipo kusema nani amewaagiza kuyapeleka.

Emmanuel ameiomba halmashauri kwenda kuyaondoa magodoro hayo na kuyafanyia vipimo kwani yanatishia   amani kwa wananchi wa kata hiyo kutokana na kuhofu kuwa  huenda yanasumu ama madhara kwa binadamu.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa kahama ABEL SHIJA amemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ANDERSON MSUMBA kuhakikisha yanaondolewa kwenye kituo hicho cha afya na kupelekwa kituo cha Polisi kwa hatua za kupata RB na kufanya upelelezi kubaini nani aliyeyapeleka katika kituo hicho.

Akijibu  kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Kahama,  Kaimu Mganga mkuu wa  halmashauri hiyo Dokta LUCAS DAVID amesema ofisi yake inataarifa na jambo hilo ambapo tayari wameanza mchakato wa kuyafuatilia ili kufahamu yamepelekwa na kampuni au na mtu gani katika kituo hicho cha Afya na kwamba wamekwisha litaarifu  jeshi la Polisi wilayani Kahama kwaajili ya uchunguzi zaidi.

MATUKIO KATIKA PICHA:

 BAADHI YA VIONGOZI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WAKIFUATILIA MAKASHABLASHA YA AJENDA.

 BAADHI YA WAKUU WA IDARA NA WANANCHI WALIOHUDHULIABARAZA HILO WAKIWA KATIKA CHUMBA CHA MKUTANO.

 MADIWANI WA KATA ZA HALMASHAURI YA KAHAMA MJI WAKIPITIA MAKASHABLASHA YA AJENDA.

 MADIWANI WAKIWA MAKINI KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI KUFUATILIA AJENDA ZA KIKAO.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) THOMAS MNONGA AKIWASISITIZA WAKUU WA IDARA WA HALMASHAURI YA KAHAMA MJI KUTUMIA RADIO ZA KIJAMII ZILIZOPO KAHAMA KUTOA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA WADOGO NA SIYO KUTUMIA NGUVU ZA MGAMBO MARA KWA MARA.
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata