WANUFAIKA WA TASAF KAHAMA WAOMBA KUTEMBELEWA NA MABWANA MIFUGO KWANI MIFUGO YAO INAKUFA KWA KUKOSA USHAURI WA KITAALAMU.

 BAADHI YA WANUFAIKA WA TASAF WAKIWA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA UFALA.
KAHAMA
Baadhi ya wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) katika kijiji cha Ufala kata ya Kilago wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameomba maafisa mifugo kuwatembelea mara kwa mara ili kuwapa elimu ya ufugaji bora na ushauri wa matibabu ya mifugo.


Wakiongea na Kijukuu Blog kijijini hapo baddhi ya wanufaika hao wamesema kuwa mifugo mingi waliyonunua kupitia fedha za TASAF imekufa kutokana na kukosa ushauri wa kitaalamu pamoja na dawa za chanjo.

Wameongeza kuwa wanashindwa kununua dawa za kutibu mifugo yao kutokana na kiasi wanachopata kutoka katika mpango TASAF kutotosheleza mahitaji yote kwani wengi wao wananunua chakula na kusomesha watoto na kuiomba serikali kuwapatia chanjo bure ili kunusuru mifugo yao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Underson Msumba amewataka wanufaika wa mradi wa TASAF ambao wana mifugo kuorodhesha majina na mahitaji yao ya chanjo ili serikali iweze kuwapatia.

Sambamba na hayo amewataka maafisa mifugo wa kata katika halmashauri ya mji wa Kahama kuwatembelea wafugaji na kuwapa ushauri na kuacha tabia ya kukaa ofisini.


Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa sasa upo katika mpango wa mradi wa tatu wa kuziwezesha kaya masikini kuunda vikundi vya kuweka akiba na kuanzisha shughuli za kiuchumi ili kujionezea kipato.

MATUKIO KATIKA PICHA:
MMOJA KATI YA MAAFISA MAENDELEO WALIOPATA MAFUNZO YA NAMNA YA KUANZISHA VIKUNDI AKITOA ELIMU KWA WANUFAIKA WA TASAF KATIKA KIJIJI CHA UFALA KATA YA KILAGO
 

MKUTANO WA HADHARA UKIENDELEA KATIKA KIJIJI CHA UFALA WILAYANI KAHAMA

BAADHI YA MAAFISA MAENDELEO NA VIONGOZI WA KIJIJI CHA UFALA WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO.
BAADHI YA WAZEE AMBAO NI WANUFAIKA WA TASAF WAKIWA KATIKA MKUTANO WA HADHARASAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata