WANAFUNZI WAFARIKI KWENYE AJALI YA BASI KAGERA

Watoto wawili ambao ni wanafunzi wamefariki dunia leo Jumamosi Aprili 28,2018 kwa kugongwa na basi la Kampuni ya Frester basi lenye namba za usajili T720 DEV katika eneo la Katongo Luranda Bukoba mkoani Kagera na kisha gari hilo kupinduka. 
Kamanda wa Polisi mkoani humo Agustine Olomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo amesema watoto hao wawili walikuwa wanaelekea shule ndipo wakagongwa na basi hilo na kudai kuwa wamefanikiwa kumkamata dereva wa basi hilo.
Aidha Kamanda Olomi amesema kuwa majeruhi zaidi wa 20 ambao walikuwa kwenye basi hilo wamepelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa matibabu zaidi kutokana na majeraha waliyoyapata.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata