WALIMU SHULE YA MSINGI MALUNGA WILAYANI KAHAMA WAANZA MPANGO WA KUWAPA UJI WANAFUNZI.


 PICHA HII SI RASMI

Shule ya Msingi Malunga katika Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga itaanza kutoa huduma ya uji  na chakula cha mchana kwa wanafunzi wake, kupitia miradi ya maendeleo inayoendeshwa na shule hiyo.

Akizungumza kwenye kipindi cha Raha ya leo cha Kahama fm, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo BITRICE KATAMA amesema  wameanzisha mradi wa kilimo  cha mbogamboga ambapo watakuwa wakiuza na kujipatia fedha kwaajili ya kununua chakula cha wanafunzi.

Amesema Mradi huo unatekelezwa baada ya kupata msaada wa  shilingi milioni 1.5 kutoka Shirika lisilo la kiserikali la EQUIP TANZANIA na kwamba wazazi na walezi wanapaswa kushirikiana na uongozi wa shule ili kuimarisha mradi huo.

Nao walimu wasimamizi wa mradi huo,  wamesema mbali na kupata chakula mradi huo utasaidia kuwajengea uwezo wanafunzi kuhusu stadi za kazi na kwamba  wamekusudia kupanua  mradi huo  pamoja na kusogeza  huduma ya maji  ya bomba.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema pindi watakapoanza kupata chakula shuleni itawasaidia  kujiimarisha kitaaluma na kuwataka wazazi nao washiriki katika mradi huo.

Afisa Elimu   elimu vifaa na Takwimu  wa halmashauri ya Mji wa Kahama, PEREPETUA  MAYIGE amesema wameanzisha mpango wa uzalishaji mali katika shule mbalimbali za msingi katika halmashauri hiyo kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi na hivyo kusaidia upatikanaji wa chakula shuleni.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata