WAKUU WA IDARA WANNE WASWEKWA RUMANDE KWA KUMDANGANYA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE MKOANI GEITA.

Wakuu wanne wa idara ambao waliodaiwa kutoa taarifa zinazotofautiana za miradi ya Wilaya ya Nyang'hwale Mkoa wa Geita kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Charles Kabeho wamewekwa rumande tangu jana mchana kwa mahojiano zaidi.

Wakuu hao ni wa idara ya elimu, kilimo, maji na maendeleo ya jamii ambao taarifa zao za fedha za miradi zilitofautiana na taarifa ya mkoa.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale, Hamimu Gwiyama amesema wakuu hao wa idara wameripoti polisi kwa mahojiano na kuwekwa ndani hadi pale watakapomaliza kuhojiwa.

"Wamewekwa ndani ili waandike maelezo ya kuonyesha kiini ni nani chanzo cha taarifa hizo kupishana na hata wakimtaja mtu mwingine tutamuongeza na atahojiwa walichokifanya ni uzembe na wameidhalilisha Serikali," amesema Gwiyama.

Gwiyama amesema wakuu hao wa idara wamewekwa ndani kuanzia jana saa nane mchana na baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi watahojiwa mmoja mmoja na kamati ya ulinzi na usalama

Amesema baada ya kukamilisha mahojiano hayo watapendekeza aina ya adhabu inayowastahili na kuipeleka kwa katibu tawala wa mkoa kutokana na makosa waliyoyafanya.


Aprili 3, 2018 Kabeho alikataa kuzindua miradi minne wilayani humo.
Miradi hiyo ni mradi wa maji, mradi wa kilimo cha matikiti, mradi wa vyumba 10 vya madarasa na mradi wa nyumba 10 bora ambayo taarifa za fedha zilipishana na taarifa za mkoa.

Miradi hiyo ni mradi wa maji, mradi wa kilimo cha matikiti, mradi wa vyumba 10 vya madarasa na mradi wa nyumba 10 bora ambayo taarifa za fedha zilipishana

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata