WAKULIMA WA PAMBA KAHAMA,WAGOMEA UTARATIBU WA KUPIMA PAMBA MARA MBILI.

MWENYEKITI WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA WILAYA KAHAMA (KACU) EMMANUEL CHEREHANI ALIYESIMAMA MBELE AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAKULIMA WA PAMBA KATIKA MKUTANO HUO.

KAHAMA
WAKULIMA wa zao laPamba katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameiomba Serikali kubadili mfumo wa ununuzi na upimaji na  wa zao hilo ili mkulima na mnunuzi wapime pamba mara moja na kukabidhiana ili kumaliza tatizo la upotevu wa kilo unaosababisha migogoro.

Hayo yamebainishwa leo na wakulima hao katika mkutano wa viongozi wa vyama vya msingi vya  pamba uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za chama kikuu cha ushirika KACU.

Wamesema kuwa zao la Pamba limekuwa na migogoro ya mara kwa mara kutokana na ubadhilifu wa kupungua kwa kilo kutokana na kupima zao hilo mara mbili kwenye chama cha msingi na makampuni yanayonunua pamba.

Wameongeza kuwa baadhi ya mawakala wa makampuni ya unununuzi wamekuwa si waaminifu kwani wamekuwa wakipunguza kilo na kuweka michanga hali inayoondoa uaminifu na kusababisha migogoro kati ya wakulima na wanunuzi.

Akipokea ombi hilo mwenyekiti wa Chama kikuu cha wakulima KACU Emmanuel Cherehani amesema kuwa atakutana na Wanunuzi wa zao la pamba,Viongozi wa bodi ya pamba,Wakurugenzi wa halmashauri husika na maafisa ushirika ili kulijadili na kumaliza swalahilo.

Hivi karibuni  Serikali kupitia Waziri mkuu Cassim Majaliwa imepitisha agizo la zao la pamba kuuzwa katika vyama vya Msingi na mnunuzi kutakiwa kulipa kwa njia ya Benki kisha chama cha msingi kimlipe mkulima mmoja mmoja kupitia akaunti yake ya benki.


 MATUKIO KATIKA PICHA
BAADHI YA VIONGOZI WA VYAMA VYA MSINGI VYA WAKULIMA WA PAMBA WAKIMSIKILIZA MWENYEKITI WA KACU HAYUPO PICHANI.

 MWENYEKITI WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA WILAYA KAHAMA (KACU) EMMANUEL CHEREHANI ALIYESIMAMA AKIWAELEZA VIONGOZI WA VYAMA VYA MSINGI VYA WAKULIMA WA PAMBA MAAGIZO YA SERIKALI YALIYOTOLEWA NA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH CASSIM MAJALIWA KUHUSU KUANZA KUNUNUA TUMBAKU KWENYE VYAMA VYA MSINGI,


KAIMU AFISA USHIRIKA WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA LIBERIA SABIN AKIWAELEWESHA WAKILIMA WA ZAO LA PAMBA NAMNA YA KUFUFUA VYAMA VILIVYOKUFA NA MIENENDO YA USHIRIKA.

MAGANGA EMMANUEL SHIJA KUTOKA KACU AKISISITIZA JAMBO KATIKA AJENDA ZILIZOPO.

 AFISA WA BENKI KUTOKA BENKI YA CRDB BEATUS TESHA AKIWAELEKEZA WAKILIMA WA PABA NAMNA YA KUFUNGUA AKAUNTI YA CHAMA CHA USHIRIKA NA AKAUNTI YA MKULIMA BINAFSI.

 AFISA WA BENKI KUTOKA BENKI YA CRDB BEATUS TESHA AKIWAONYESHA WAKULIMA MFANO WA PICHA INAYOTAKIWA KATIKA KUFUNGUA AKAUNTI.


WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA WAKIENDELEA KUWASIKILIZA MAAFISA USHIRIKA WALIOKUWA WANAWAPA ELIMU.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata