WAJAWAZITO MARUFUKU KUTUMIA MAJI YA VISIMA KARIBU MIGODI

Na James Timber, Mwanza
Mama wajawazito wenye makazi yao jirani na migodi hapa nchini wameshauriwa kutotumia vyanzo vya maji vilivyopo katika maeneo hayo, kutokana na kuwa na kemikali zinazopelekea kuzaa watoto wenye mdomo sungura.

Hayo yalisemwa na  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure Mwanza  Dk. Bahati Msaki wakati wa uzinduzi wa opresheni ya midomo sungura kwa wakazi wa Mikoa ya Kanda ya ziwa.

Dk. Bahati alisema tatizo hilo limekuwa kubwa hasa kwa Mkoa wa Geita kutokana na eneo hilo kutoka wagonjwa wengi wenye tatizo hilo, kutokana na kuwepo kwa migodi mingi.

"Nashukuru uwepo wa Taasisi ya Rafiki Segical Mission ambayo ndo wataalamu wa kuendesha opresheni hiyo bure kutoka nchini Australia kwa muda wa miaka tisa na tayari wameishatoa huduma hiyo kwa watu 900 bure.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela aliwapongeza Urafiki Sagical Mission kwa mchango wako kwani huduma hiyo itachangia kupunguza tatizo hilo.

Aidha aliupongeza Mgodi wa Dhahabu wa GGM na Accacia kwa kubeba jukumu la kuwasafirisha watoto hao bure kutoka mikoa mbalimbali ikiwa na kuwagharamikia kila kitu kwa kipindi hiki wanapokuwa mkoani hapa.

Taasisi hiyo kwa kipindi cha siku 10 inatarajia kufanya opresheni 60 kwa awamu ya kwanza na kwa awamu ya pili  watoto 60 jumla 120 na watu wenye tatizo la kuungua na moto na kuwa na makovu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata