VODACOM WATOA BAISKELI 22 KWA VIJANA WAO WANAOSAJILI LINE MITAANI MJINI KAHAMA.


MKUU WA MAUZO YA KANDA WA KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA DOMICIAN MKAMA AKIMKABIDHI BAISKELI YAKE BINTI SARAFINA KHAMIS.

KAHAMA
Kampuni ya simu za mkoni ya Vodacom Tanzania leo imekabidhi  jumla ya baiskeli 22 kwa vijana  wake wanaofanya kazi za kusajili Laini katika maeneo mbalimbali wilayani Kahama kwa lengo la kuwafikia wananchi na kutoa huduma kirahisi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi  baiskeli hizo, Mkuu wa mauzo ya Kanda  wa  Kampuni ya Vodacom Tanzania, Domician Mkama amesema kutokana na kutambua mchango mkubwa wa vijana kujituma na kueneza huduma katika maeneo mengi ikiwamo vijijini.

Aidha amewataka vijana hao kuwa makini katika kuzitumia baisikeli hizo  kwa kuzingatia usalama barabarani ili wasiwe chanzo cha ajali na kwamba Vodacom itaendelea kutoa motisha kwa vijana na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa  biashara wa Vodacom, kanda ya Kahama Jovin Ikate amesema wafanyakazi wa kampuni hiyo hasa kanda ya Kahama kufanya kazi kwa bidii na kuongeza uaminifu ili kuendelea kuleta mafanikio kwao kwa kampuni ya Vodacom na taifa kwa ujumla.


Nao baadhi ya vijana waliokabidhiwa baiskeli hizo wameipongeza Kampuni ya Vodacom Tanzania na kuahidi kuongeza bidii katika kazi na kwa wateja.

MATUKIO KATIKA PICHA:

BAADHI YA VIJANA WANAOFANYA KAZI YA KUSAJILI LAINI KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA MJI WA KAHAMA WAKIWA WAMEKETI KATIKA NAFASI ZAO WAKISUBIRI KUKABIDHIWA BAISKELI NA VYETI VYAO.

 BAADHI YA WANANCHI WA MJI WA KAHAMA WAKIWA KATIKA BANDA LA VODACOM WAKINUNUA NA KUULIZA MASWALI MBALI MBALI KUHUSU HUDUMA ZA VODACOM NA VIFURUSHI VYAKE.

VIONGOZI WA MASOKO KUTOKA VODACOM KAHAMA WAKIWA ENEO LA TUKIO WAKISUBIRI KUSHUHUDIA TUKIO LA KUKABIDHI BAISKELI

 MENEJA BIASHARA KANDA YA KAHAMA JOVIN IKATE AMBAYE NDIYE ALIKUWA MC WA SHUGHULI NZIMA YA KUKABIDHI BAISKELI HIZO AKIENDELEA KUTOA UTARATIBU WA RATIBA YA SHUGHULI YENYEWE

 MKUU WA MAUZO YA KANDA WA KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA DOMICIAN MKAMA AKITOA NENO KWA VIJANA WALIOKABIDHIWA BAISKELI KUHUSU NAMNA YA KUWA WANAPOKUWA BARABARANI WAKATI WANAPOENDESHA BAISKELI HIZO.

 VIONGOZI WA MASOKO KATIKA MAENEO MBALI MBALI WILAYANI KAHAMA WAKIWA WAMEKETI KUSHUHUDIA TUKIO LA KUKAKABIDHIWA BAISKELI KWA VIJANA 22 WANAOFANYA NAO KAZI MAENEO MBALIMBALI.

 MKUU WA MAUZO YA KANDA WA KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA DOMICIAN MKAMA AKIFANYA ZOEZI LA KUKABIDHI VYETI KWA VIJANA ISHIRINI NA MBILI KAMA ISHARA YA KUTAMBUA MCHANGO WAO.

 BAADHI YA VIJANA WANAOFANYA KAZI YA KUSAJILI LAINI KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA MJI WA KAHAMA WAKIWA WAMEKETI KATIKA NAFASI ZAO WAKISUBIRI KUKABIDHIWA BAISKELI NA VYETI VYAO.

 MKUU WA MAUZO YA KANDA WA KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA DOMICIAN MKAMA AKIFANYA ZOEZI LA KUKABIDHI VYETI KWA VIJANA ISHIRINI NA MBILI KAMA ISHARA YA KUTAMBUA MCHANGO WAO.

 VIJANA WANAOFANYA KAZI ZA KUSAJILI LAINI KATIKA MAENEO MBALI MBALI WILAYANI KAHAMA WAKIWA WAMEPANDA KWENYE BAISKELI ZAO YATARI KWA AJILI YA KUZUNGUKA KATIKA VIUNGA VYA MJI WA KAHAMA.

 MGENI RASMI AMBAYE NI AFISA UTAMADUNI WA HALMASHAURI YA MJI AKIMKABIDHI MMOJA WA VIJANA BAISKELI YAKE.

MC IKATE AMBAYE NI MENEJA BIASHARA KANDA YA KAHAMA AKIENDELEA NA ATIBA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata