UBOVU WA BARABARA USHETU KAHAMA WACHELEWESHA MASOKO YA TUMBAKU.
 BARABARA YA KUTOKA KATA YA UBAGWE KUPITIA ULOWA HADI KAHAMA MJINI ILIVYOHARIBIWA NA MVUA.

KAHAMA
Kuharibika kwa miundo mbinu ya barabara na madaraja katika halmashauri ya Ushetu kutokana na mvua kubwa zilizonyesha wilayani Kahama kumesababisha kuchelewa kufunguliwa kwa masoko ya tumbaku tofauti na ilivyo kuwa imepangwa awali.

Akizungumza katika kikao maalumu cha Chama kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU Mwenyekiti wa chama hicho, EMMANUEL CHARAHANI amesema kuharibika kwa miundo mbinu kumesababisha kusogeza mbele kufunguliwa kwa soko hilo la tumbaku katika mkoa wa Kitumbaku, Kahama.

CHEREHANI ameongeza kuwa kusogezwa mbele kwa msimu wa masoko ya tumbaku kunaweza kusababisha ongezeko la riba kwa wanachama na hivyo kupata hasara au kupunguza kabisa faida kwa mkulima.
 MWENYEKITI WA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAHAMA (KACU) EMMANUEL CHEREHANI.

Nao baadhi ya wakulima wa tumbaku kutoka halmashauri ya ushetu wamezungumzia suala hilo la uharibifu wa miundo mbinu katika kipindi hiki cha  mvua zinapoendelea kunyesha jambo ambalo limesababisha washindwe kusafirisha mazao yao.

Akitolewa ufafanuzi changamoto hiyo, mkuu wa wilaya ya Kahama, FADHILI NKURLU amesema licha ya Wakala wa Barabara za mijiji na vijijini (TARURA) kuwa na fedha kwa ajili ya marekebisho ya barabara hizo, changamoto kubwa ni mvua zinazoendelea kunyesha na kuchelewesha marekebisho hayo.


Awali KACU ilikua inatarajia kufungua soko la tumbaku Aprili 24 mwaka huu, lakni kutokana kuharibiwa kwa barabara na mvua zinazoendelea kunyesha wamepanga kufungua soko hilo Mei 10 mwaka huu.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata