TUMIA NJIA HII RAHISI UNAYOWEZA KUITUMIA KUZALISHA KUKU CHOTARA

Ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara. Tunaposema chotara tuna maanisha ni mchanganyingo wa aina mbili za kuku. Mfano mchanganyiko wa kienyeji na kenbro wanajulikana kama kuku wa kenya.

Sifa ya kuku chotara ni kama ifuatavyo,

1. Wanastahimili sana magonjwa.
2 Wanataga mayai mengi mpaka 240 kwa mwaka kama ukiwalisha vizuri kwa miaka mitano
3. Wanakua haraka sana. Wanafikisha mpaka kilo 3 kwa muda wa miezi mitatu kama ukiwalisha vizuri
4.Anatumika kama kuku wa nyama na mayai

Ukitaka kufuga kuku kibiashara usimwachie kuku kuhatamia mayai kwani unampotezea muda wa kutaga. Kusanya mayai weka kwenye mashine ya kutotolea vifaranga. Ukitaka kupata faida kubwa usinunue chakula bali tengeneza mwenyewa kwani bei za vyakula zimepanda sana. Kwenye ufugaji asilimia 80 inaenda kwenye ulishaji na asilimia 20 inaenda kwenye madawa.

Hatua ya kwanza, andaa banda lako ambalo linafaa kwa matumizi ya ufugaji wa kuku, banda la kuku linatakiwa liwe linapitisha hewa ya kutosha.

Hatua ya pili,  andaa kuku wa kienyeji matetea (majike) na jogoo la kisasa aina ya kocks au aina yoyote ile ambayo inafaa, wachanganye kuku wa kienyeji na jogoo la kisasa katika banda moja ili uweze kupata mayayi yenye mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa. Kumbuka jogoo mmoja (1) anatakiwa kuwa na matetea kumi na tano (15) au matetea yasizidi kumi na tano.

Hatua ya tatu kutotolesha mayayi ambayo umeyapata kutokana na mchanganyiko wako, unaweza kutumia mashine za kutotolesha mayayi au unaweza kuwatumia matetea yako ya kuku wa kienyeji kuatamia mayayi yako.

Hatua ya nne baada ya siku ishirini na moja (21), vifaranga vyako vitakuwa tayari kwa kutumia matetea ya kuku wa kienyeji au mashine ya kutotolesha vifaranga kwa ajilia ya matunzo mpaka wakiwa wakubwa. Vifaranga vikishakuwa tayari chanjo muhimu wanahitaji ili kuzuia vifo na mripuko wa magonjwa. Vifaranga kwa muda wa wiki tatu hadi nne wanahitaji joto la kutosha, kwa ajili ya ukuaji afya njema.

Chanjo na dawa muhimu kwa vifaranga mpaka wakiwa wakubwa

Siku 2-6 Pullorum Trisulmycine,Trimazine 30%au Cotrim+Vitalyte,Amin’total au Broiler booster maji

Siku ya 7 Mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota maji
Siku 14 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Siku 16-20 Coccidiosis Trisulmycine/Trimazine/Esb3 30%+Dawa yoyote ya Vitamin maji
Siku 21 mdondo(newcastle) Newcastle vaccine(Lasota) maji
Siku 28 Gumboro Gumboro (Bursine vaccine-IBD) maji
Wiki ya 6-8 Ndui Fowl pox vaccine sindano kwenye bawa
Wiki ya 13 minyoo Pipperazine cirtrate+Dawa yoyote ya vitamin maji
Wiki ya 10 hadi ya 15 ukataji midomo Dawa ya vitamin itumike baada ya zoezi maji

KUMBUKA
Dawa ya minyoo na chanjo ya kideli kila baada ya miezi mitatu

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata