TASAF YAZISHAURI KAYA MASIKINI KUWEKA AKIBA NA KUANZISHA SHUGHULI ZA KIUCHUMI ILI KUJIONGEZEA KIPATO.


MTAALAMU WA MAFUNZO NA USHIRIKISHWAJI JAMII KUTOKA TASAF MAKAO MAKUU BI MERCY MANDAWA

KAHAMA
Jamii nchini hasa zinazotoka katika kaya masikini zimetakiwa kuweka akiba na kuanzisha shughuli ndogo ndogo za kiuchumi ili kujiongezea kipato na kuondokana  na  hali ya kuwa tegemezi katika jamii.

Wito huo umetolewa leo na mtaalamu wa mafunzo na ushirikishwaji jamii kutoka TASAF makao makuu Bi Mercy Mandawa katika ufunguzi wa semina ya siku tano inayolenga kuwajengea uwezo wawezeshaji wa mpango wa kusaidia kaya masikini kutoka halmashauri za Kahama mjini na Mbogwe.

Bi Mandawa amesema amesema jamii zinazotoka  kwenye kaya masikini haziwezi kuona faida za pesa zinazotolewa na TASAF ikiwa hawatojiwekea utaratibu wa kujiwekea akiba ikiwa ni pamoja na kuanzisha shuguli za kiuchumi ili kukuza kipato.

Sambamba na hayo Mandawa ametoa wito kwa wawezeshaji wa mpango wa kusaidia kaya masikini kutoa elimu ya kina kuhusu uuandaji na umuhimu wa vikundi ili kuzisaidia kaya masikini kutambua umuhimu wa vikundi katika Shughuli za maendeleo.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo ambao ni maafisa maendeleo wa Kata kutoka halmashauri za Kahama mjini na Bukombe wamesema kuwa mafunzo waliyopata watayatumia vizuri na kwamba watawasaidia kaya masikini kuanzisha vikundi na shughuli za kiuchumi.

Mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa sasa upo katika mpango wa mradi wa tatu wa kuziwezesha kaya masikini kuunda vikundi vya kuweka akiba na kuanzisha shughuli za kiuchumi ili kujionezea kipato.
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata