TANESCO KAHAMA LAWAMANI,WAKAZI WA MTAA SANGO NYASUBI WALIA KUKOSA UMEME WIKI NZIMA.


Wakazi wa kata ya Nyasubi mtaa wa Sango wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamelilalamikia shirika la Umeme (TANESCO) kwa kushindwa kurejesha huduma ya umeme kwenye makazi yao kwa zaidi ya wiki moja sasa.
Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti na KAHAMAFM wakazi hao wamesema tatizo la kukosekana kwa umeme katika mtaa huo limedumu kwa zaidi ya wiki moja na kusababisha shughuli zao zinazo tegemea umeme kusimama.

Wameongeza kuwa kukosekana kwa umeme kumesababisha kuwepo kwa vibaka,kufunga ofisi zao kama saluni,karakana hali inayopelekea kukosa mapato ya kila siku.

Kwa upande wake meneja wa shirika la ugavi wa umeme Tanzania (TANESCO) KING FOKANYA, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo katika mtaa huo na kusema sio mtaa wote, tatizo hilo wanalishughulikia ili kurejesha huduma hiyo muhimu kwa wananchiSAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata