SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LATOA MSAADA WA VIFAA KATIKA DAWATI LA JINSIA POLISI KAHAMA.

MENEJA WA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA SAVE THE CHILDREN MKOANI SHINYANGA BENETY MALIMA KUSHOTO AKIKMKABIDHI SAMANI AFISA WA DAWATI LA JINSIA KAHAMA INSPEKTA ELIAS SIKANDA

KAHAMA
Jeshi la polisi kitengo cha jinsia na watoto wilayani Kahama mkoani Shinyanga limesema litaendelea kuweka mazingira  rafiki kwenye kitengo hicho ili jamii iweze kuripoti  taarifa na matukio  ya ukatiri wa kijinsia kwenye kitengo hicho bila woga wowote.

Hayo yamesemwa leo mjini Kahama na  Afisa wa dawati la jinsia na watoto wilayani humo,  Inspekta..ELIAS SIKANDA wakati wa kupokea  samani  mbalimbali  zilizotolewa na shirika lisilo la kiserikali linaloshugulikia  masuala ya watoto SAVE THE CHILDREN.

Amesema kitengo hicho kimezidi kuimarisha mazingira ya kazi na hivyo jamii wanapaswa kutumia dawati hilo kutoa taarifa za ukatiri wa kinjisia na watoto na kwamba  msaada waliopewa na  Shirika la SAVE THE CHILDREN  utasaidia katika ukamilishaji wa kesi  mbalimbali katika  dawati hilo.

Naye Meneja wa SAVE THE  CHILDREN   mkoa wa Shinyanga BENETY MALIMA amesema wataendelea kushirikiana na kitengo hicho katika kutokomeza tatizo la ukatili wa kijinsia na watoto katika jamii na kwamba jamii iwe na uelewa wa kutumia dawati la jinsia na watoto kupata haki zao za msigi.

Vifaa vilivyotolewa  na   shirika hilo ni pamoja na Meza, viti mabenchi ya chuma na   vifaa vya kuchezea watoto  vinavyotumika  kuwapa watoto kwaajili ya kurahisisha upelelezi wa kesi vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 2.7

MATUKIO KATIKA PICHA:


JENGO LA OFISI ZA DAWATI LA JINSIA KATIKA KITUO CHA POLISI KAHAMA.

GARI LA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LIKIWA LIMEWASILI KULETA VIFAA AMBAVYO VIMEKABIDHIWA KATIKA KITUO CHA DAWATI LA JINSIA KAHAMA.

MAAFISA WA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN WAKIFANYA MAKABIDHIANO YA NYARAKA ZINAZOHUSU VIFAA WALIVYOTOA.

MAAFISA WA POLISI KITENGO CHA DAWATI LA JINSIA WAKISIKILIZA KWA UMAKINI UFAFANUZI WA MAAFISA WA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN KUHUSU VIFAA VILIVYOTOLEWA.

MENEJA WA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA SAVE THE CHILDREN MKOANI SHINYANGA BENETY MALIMA KUSHOTO AKIKMKABIDHI SAMANI AFISA WA DAWATI LA JINSIA KAHAMA INSPEKTA ELIAS SIKANDA

VIFAA MAALUMU KWA AJILI YA KUCHEZEA WATOTO VILIVYOTOLEWA KATIKA KITUO CHA DAWATI LA JINSIA POLISI KAHAMA.

MENEJA WA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN AKIWA NA MAAFISA WA POLISI DAWATI LA JINSIA WAKIAANGALIA VIFAA MAALUMU KWA AJILI YA KUCHEZEA WATOTO.

VIFAA VYA KUCHEZEA WATOTO VILIVYOKABIDHIWA KATIKA DAWATI LA JINSIA KAHAMA.

MENEJA WA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA SAVE THE CHILDREN MKOANI SHINYANGA BENETY MALIMA KUSHOTO AKIWAONYESHA MAAFISA WA POLISI NAMNA AMBAVYO ANAWEZA KUCHEZEA VIFAA HIVYO. 

AFISA WA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN ALIYESIMAMA AKIANGALIA UKAMILISHAJI WA UJAZAJI WA FOMU MAALUMU YA KUKIRI KUPOKEA VIFAA

AFISA WA DAWATI LA JINSIA KAHAMA INSPEKTA ELIAS SIKANDA AKIVIPANGA VIFAA VYA KUCHEZEA WATOTO VILIVYOKABIDHIWA NA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN

MAAFISA WA POLISI KITENGO CHA DAWATI LA JINSIA WAKIFURAHI KUPATA VIFAA AMBAVYO WANAAMINI VITAWASAIDIA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.

PICHA YA PAMOJA BAADA YA ZOEZI LA KUKABIDHIANA VIFAA KUKAMILIA.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata