SERIKALI KUSAMBAZAHUDUMA YA CHF NCHI NZIMA,SASA WATU SITA KUTOA SHILINGI ELFU 30.

Serikali  imeimarisha mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa  ambapo katika mwaka wa fedha 2018/19 imekusuduia kusambaza huduma ya CHF  kwenye mikoa yote  nchini.

Akizungumza leo kwenye baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Kwa niaba ya Mkurugunzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya halmashauri hiyo, Dokta LUCAS DAVID amesema tayari serikali imetoa maelekezo  katika halmashauri zote nchini.

Amesema  huduma hiyo imeonekana kufanya vizuri katika  mikoa mitatu ya awali  na kwamba  kwa sasa huduma hiyo itapatikana kwa shilingi elfu 30 kwa watu sita badala ya elfu 10  huku elimu itaendelea kutolewa kwa wananchi wote.

Katika hatua nyingine Dokta LUCAS amesema  hospitali ya Mji wa Kahama imekusudia kuongeza  maduka ya dawa ya kutoa dawa  kwa wateja wa bima ya Afya  katika maeneo mbalimbali   mjini Kahama ili kuboresha huduma hiyo kwa sasa.

c

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata