RAIS MAGUFULI: MKE WANGU NI MTOTO WA POLISI, MAISHA YAO NAYAJUA

Rais John Magufuli leo ametoboa siri kuwa mke wake, Janeth alikuwa ni mtoto wa polisi.

Ameyasema hayo leo Aprili 7 wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi mjini Arusha na kusema baba mkwe wake alikuwa sajenti wa polisi.
“Nyumba za polisi ndizo zimenipa mke kwa hiyo nyumba za polisi ninazifahamu, huyu mke wangu niliye naye alikuwa mtoto wa polisi, marehemu baba yake hakuwa na cheo kikubwa alifariki akiwa sajenti,” amesema.
Ameongeza kuwa, “Ingekuwa nazindua Moshi, angenionyesha nyumba walizokaa lakini za Oysterbay alizoishi alishanionyesha na za Ukonga na za sehemu nyingine. Kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu.”

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata