RAIS KAGAME AMPOGEZA MEYA WA JIJI LA MWANZA

Na James Timber, Mwanza
Rais wa Rwanda Paul Kagame ametuma salamu za pongezi kwa Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire kwa kuanzisha vituo vya Alliance vinavyotoa taaluma na kuendeleza vipaji vya soka.

Akizungumza na Wandishi wa Habari jijini Mwanza Wakala wa Michezo ambaye pia ni Balozi wa Michezo nchini Rwanda Gakumba Patrick alisema kuwa  Rais Kagame amemuomba Mkurugenzi wa Alliance kuwekeza nchini Rwanda.

"Rais amefurahishwa na Shule za Alliance zinazofanya vizuri kitaaluma na michezo, amenituma kumuomba Mkurugenzi kushirikiana na nchi ya Rwanda katika uwekezaji kwa lengo la kukuza na kuimarisha uchumi wa Afrika Mashariki.

Gakumba, alisema kuwa Watanzania wanapaswa kumshukuru Meya huyo kwa kuwainua vijana wengi katika mchezo wa soka na taaluma nzuri itolewao katika Shule ya za Alliance Sports Academy.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Mwanza alisema kuwa yupo tayari kutumia fursa ya kuwekeza nchini Rwanda kwa lengo la kupiga hatua mbele ya kiuchumi.

Pia Bwire amewakaribisha vijana kutoka Rwanda kujiunga na vituo hivyo lengo likiwa ni  kupata taaluma bora  na kuendeleza vipaji vya soka.

Aidha alitoa shukrani kwa Rais Dk. John Magufuli kwa kufungua milango ya fursa baada ya ziara yake nchini Rwanda.

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata