ORODHA YA MAJINA YA WAANDISHI WA HABARI WATEULE TUZO ZA UMAHIRI WA UANDISHI WA HABARI - EJAT 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WATEULE WA EJAT 2017

Dar es Salaam, Aprili 18 2018

Jopo la majaji nane lililokaa kuanzia April 4 hadi 11, 2018 kupitia jumla ya kazi za kiandishi 545  zilizokuwa katika makundi 16 ya kushindaniwa katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2017, limemaliza kazi yake. 


Jopo liliongozwa na mwenyekiti wake, Ndimara Tegambwage. Wajumbe wake wengine walikuwa  Rose Haji (Katibu), Hassan Mhelela, Hamis Mzee, Selemani Mpochi, Pudenciana Temba, Kiondo Mshana na James Gayo. Majaji  waliapishwa  na  Rais wa Baraza la Habari Tanzania,  Jaji Thomas Mihayo Machi  29,  2018 kabla ya kuanza kazi hiyo. 

Majaji hao wameteua jumla ya waandishi 49 ambao wataingia katika kinyang’anyiro cha mashindano ya EJAT 2017.  Kati ya wateule hao 49, wateule 30 wanatoka katika magazeti; 10 wanatoka redio na 9 wanatoka televisheni.
  
Idadi ya wateule wa EJAT mwaka huu ina wanawake 24 ambayo ni asilimia 49 ikiwa ni ongezeko la asilimia 19 kulinganisha na mwaka jana ambapo wanawake walikuwa asilimia 30 ya walioingia kwenye kinyang’anyiro hiki mwaka jana.

Katika EJAT 2016 wateule walikuwa 66, kati yao 36 walitoka kwenye magazeti, 16 kutoka radio na 14 kutoka runinga. 

Jumla ya kazi 545 zilipokelewa katika msimu huu wa tisa wa EJAT 2017, ambapo kazi 339 zilitoka kwa waandishi wa habari wa wanaume sawa na asilimia 62.2, wakati wanawake waliwasilisha kazi 206 ambazo ni sawa na asilimia 37.8 ya kazi zote zilizowasilishwa. 

Ifuatayo ni orodha ya makundi yaliyoshindaniwa.

1. Uandishi wa Habari za Biashara, Uchumi na Fedha;
2. Uandishi wa Habari za Michezo na Utamadumi;
3. Uandishi wa Habari za Afya;
4. Uandishi wa Habari za Kilimo na Biashara za Kilimo;
5. Kundi la Uandishi wa Habari za Elimu;
6. Kundi la Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi;
7. Kundi la Uandishi wa Habari za Uchunguzi;
8. Kundi la Uandishi wa Habari za  Takwimu;
9. Kundi la Uandishi wa Habari za Haki za Binadamu na Utawala Bora;
10. Mpiga picha Bora – Magazeti;
11. Mpiga picha Bora  – Runinga;
12. Mchora Kanuni Bora;
13. Kundi la Uandishi wa Habari za Jinsia na Vijana;
14. Kundi la Uandishi wa Habari za Wazee;
15. Kundi la Uandishi wa Habari za Kodi na Mapato;
16. Kundi la  Wazi.

Ifuatayo ni orodha ya wateule wa EJAT 2017 pamoja na vyombo vyao:  

Haya hapa Majina ya wateule na  Chombo cha Habari

1 Bernard James The Citizen

2 Jane Shirima Azam Two

3 Devotha John The Citizen

4 Hawa Bihoga DW

5 Sophia Mgaza Azam Two

6 Abdul Kingo  Nipashe

7 Vivian Pyuza CG FM

8 Anne Robi Dailynews

9 Faraja Sendegeya AZAM TV

10 Theodora Mrema STAR TV

11 Calvin Gwabara SUA FM

12 Jamaly Hashim AZAM TV

13 Salome Kitomary Nipashe

14 Sebastian Kolowa ITV

15 Godfrey Monyo ITV

16 Leonard Mapuri STAR TV

17 Sauli Giliad Habari Leo

18 Godfrey Nago TBC1

19 Imani Makongoro Mwanasport

20 Omar Fungo Mwananchi

21 Jumanne Juma Mtanzania

22 Nuzulack Dausen The Citizen

23 Saumu Mwalimu The Citizen

24 Adrian Mgaya Mlimani TV

25 Peter Rogers ITV

26 Harieth Makweta Mwananchi

27 Gerald Kitabu The Guardian

28 David Chikoko Guardian

29 Rahma Suleiman Ali Nipashe

30 Dino Mgunda STAR TV

31 Musa Siwayombe Mwananchi

32 Hamis Hollela TBC Taifa

33 Abdul Mitumba Nipashe

34 Projestus Binamungu RFA

35 Yohan Gwangway STAR TV

36 Elias Msuya Mwananchi

37 Penina Kajura HHC radio

38 Alexander Sanga Dailynews

39 Maloda Mandago Nipashe

40 George Kasembe TBC1

41 Nora Damian Sam  Mtanzania

42 Hellen Nachilongo The Citizen

43 Muhidin Msamba Guardian on Sunday

44 Maajabu Ally Pangani FM

45 Tumaini Msowoya  Mwananchi

46 Anuary Mkama DW

47 Ericky Boniphace Mwananchi

48 Octavian Galakwila Azam TV

49 Aurelia Gabriel Kwizera Radio

--------------------------------
Kajubi D. Mukajanga  
Mwenyekiti
Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2017

SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata