NEEMA YATUA KAHAMA: CHUO KIKUU HURIA (THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA) CHAFUNGULIWA RASMI.

MAKAMO MKUU WA CHUO W CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA PROFESA ELIUS TOZO BISANDA AKIZUNGUMZA NA WADAU WA ELIMU KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO ILIPOKUWA HALMSHAURI YA MJI WA KAHAMA.

KAHAMA

SERIKALI  wilayani Kahama mkoani Shinyanga  imesema uwepo wa chuo kikuu huria  (THE OPEN UNIVESITY OF TANZANIA) katika mji wa Kahama ni fursa na neema kwa wananchi wilayani humo wanaohitaji kujiendeleza na elimu ya chuo kikuu katika fani mbalimbali.

Akizungumza leo kwenye ufunguzi  wa tawi la Chuo kikuu huria   mjini Kahama, kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kahama FADHIL NKURLU, Kaimu  katibu tawala wa wilaya hiyo TUMSHUKURU  MDUI amewataka wananchi kukutumia chuo hicho kwa manufaa yao ya kielimu na uchumi.

Amesema  uwepo kwa chuo hicho katika wilaya ya Kahama  kitatoa nafasi kubwa kwa vijana na wananchi kwa ujumla, kujiendeleza  katika fani wanayoihitaji pasipo kuathiri shughuli zao za kila siku.

MDUI amesema seriakali  wilayani humo itaendelea kutoa ushirikiano kwa  chuo kikuu  hicho katika kuhamasisha  wananchi kukitumia chuo hicho  na kusimmamia  mahitaji muhimu kwa chuo hicho na wanafunzi watakaokuwa wanasoma chuoni hapo.

Naye Makamo  mkuu wa  chuo kikuu huria  Profesa Elius Tozo Bisanda amesema  kwa sasa wanaendelea kuongeza vifaa vingine kwaajili ya wanafunzi kupata taaluma  na kufanya mithani katika tawi hilo na kwamba lengo la chuo hicho ni kusogeza  karibu huduma ya masomo ya chuo kikuu  kwa wanafunzi kule walipo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  mipango na Maendeleo wa Chuo hicho, BENJAMINI DUSU ameishukuru serikali na wananchi wa wilaya hiyo kwa kufanikisha na kukipokea chuo hicho  na kwamaba   tawi hilo limepunguza adha ya wanafunzi wa Kahama kutoka Kahama kwenda shinyanga kwenye tawi la Shinyanga.

Akizungumza kwa niaba ya serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Kiongozi wa wanafunzi wilayani Kahama Julius Chagama ameushukuru uongozi wa Chuko kikuu huria  makao makuu na kwa kusogeza tawi katika wilaya ya Kahama   hali ambayo inawapa nafasi   kubwa ya wanafunzi  kujiendeleza kujiendeleza kielimu  kupitia chuo hicho.


Chuo kikuu  Huria (OPEN UNIVESTY) tawi la Kahama kitakuwa kikitoa huduma ya masomo ya fani mbalimbali   katika   majengo yaliyokuwa yanatumiwa na Halmashauri ya Mji wa Kahama katika Mtaa wa Nyihogo mjini Kahama.

MATUKIO KATIKA PICHA:
 MEZA KUU WAKIWA WAMETULIA KUMSIKILIZA MC AMBAYE NI MKURUGENZI WA MAWASILIANO NA MASOKO WA CHUO HICHO DR MOHAMED OMARY HAYUPO PICHANI.

 VIONGOZI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WA WILAYA WAKIJITAMBULISHA KATIKA GHAFLA HIYO YA UZINDUZI WA TAWI LA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA.

 VIONGOZI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WA WILAYA WAKIJITAMBULISHA KATIKA GHAFLA HIYO YA UZINDUZI WA TAWI LA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA.

 KAIMU KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA TUMSHUKURU MDUI AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MKUU WA WILAYAYA KAHAMA.

 MAKAMO MKUU WA CHUO W CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA PROFESA ELIUS TOZO BISANDA.

 MMOJA WA WANAFUNZI WANAOSOMA KATIKA CHUO KIKUU HURIA BWANA JULIUS CHAGAMA AKITOA SHUKRANI KWA UONGOZI WA CHUO KWA KUSOGEZA HUDUMA HIYO KARIBU.

MKURUGENZI WA MIPANGO NA MAENDELEO WA CHUO HICHO BENJAMINI DUSU AKITETA JAMBO KATIKA UFUNGUZI HUO.
SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata