MZEE MAJUTO ALAZWA TENA HOSPITALI BAADA YA KUZIDIWA

Muigizaji na mchekeshaji wa siku nyingi, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto, amelazwa tena katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa.

Mke wa mwigizaji huyo, Aisha Yusufu amesema walimpeleka mume wake  hospitalini hapo leo Aprili 23,201 saa 7:00 mchana.

Aisha amesema kidonda alichofanyiwa upasuaji kimeleta shida, hivyo kumpeleka kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Majuto alilazwa hospitalini hapo Januari mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa tezi dume.


SAMBAZA HABARI HII
Habari Iliyopita
Habari Inayofuata